Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule za Igamba na Itaka kwa ajili ya kuanza kidato cha tano na sita?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Ni kweli Shule ya Sekondari Igamba imepokea wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita, lakini Jimbo la Mbozi ndiyo linaloongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ndani ya Mkoa wa Songwe. Tupo wakazi laki tatu, lakini tuna shule za sekondari 28 na tuna high school moja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni kwamba kuna haja ya msingi ya kupeleka fedha kwa haraka ili hii Shule ya Sekondari ya Itaka ianze nayo kuwa high school na kupokea wanafunzi? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafanya uwekezaji mkubwa sana kwenye upande huu wa kuimarisha miundombinu ya Sekta ya Elimumsingi, lakini kuhakikisha Sekta ya Elimumsingi kwa ujumla wake inaweza kuendelea kuimarika ili wanafunzi wetu wapate elimu iliyo bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika upande wa miundombinu, Serikali kama nilivyotangulia kusema katika Jimbo hili la Mbozi, tayari imefanya uwekezaji wa kujenga miundombinu inayohitajika kwa ajili ya kupandisha shule moja hii ya Sekondari ya Igamba iweze kuwa shule ya kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali tayari imeweka katika mipango ujenzi wa miundombinu muhimu na uimarishaji wa Shule hii ya Sekondari ya Itaka ili na yenyewe iweze kupandishwa hadhi kuwa kidato cha tano na cha sita ili iweze kuwanufaisha wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kutumia nafasi hii kumkumbusha Mkurugenzi wajibu wake wa msingi, kwamba kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, aweze kuweka katika mipango na kutenga bajeti kwa ajili ya kuanza kujenga miundombinu hii muhimu kabisa itakayohitajika kwa ajili ya kupandisha shule hii ya Sekondari Itaka kuwa na kidato cha tano na cha sita. Serikali Kuu itakuja kuunga mkono jitihada hizi kwa kuongeza nguvu kuhakikisha miundombinu yote inayohitajika inakamilika, na shule hii inapata usajili wa kuweza sasa kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule za Igamba na Itaka kwa ajili ya kuanza kidato cha tano na sita?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Shule ya Sekondari ya Chamriho na Shule ya Sekondari ya Hunyari zimekamilisha miundombinu yote ya kuanzishwa kwa high school kidato cha tano na kidato cha sita. Je, ni lini hizo shule zitafunguliwa; na miundombinu yote, imekamilika?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa shule za sekondari kama hizi, mathalan hii Shule ya Sekondari Chamriho na Hunyari ambazo tayari zimejengewa miundombinu ya msingi zitakazoziwezesha kuwa shule za kidato cha tano na cha sita, ni kwamba, Mkurugenzi anafanya mawasiliano na Wizara ya Elimu ili wadhibiti ubora waweze kufika kufanya ukaguzi na hatimaye shule hizi ziweze kupata usajili na wanafunzi sasa waweze kuanza kupokelewa katika shule hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba kutumia nafasi hii kumkumbusha Mkurugenzi wajibu wake wa msingi, aweze kufanya mawasiliano hayo na Wizara ya Elimu kwa ajili ya kupata usajili wa shule hizi, ziweze sasa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita.