Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 53 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 676 2025-06-25

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Shule za Igamba na Itaka kwa ajili ya kuanza kidato cha tano na sita?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikijenga na kupandisha hadhi shule za sekondari ili kutoa elimu ya Kidato cha Tano na Sita kwa kuzingatia mpango wa Halmashauri husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2018/2019 na mwaka 2023/2024 Serikali ilitoa shilingi milioni 418 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, matundu sita ya vyoo na mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Igamba na vyumba vinne vya madarasa na matundu manne ya vyoo katika Shule ya Sekondari Itaka. Aidha, mwaka 2025 shule ya Sekondari Igamba imepangiwa wanafunzi 57 wa Kidato cha Tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita katika shule za Sekondari Igamba na Itaka kadri ya upatikanaji wa fedha.