Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa Maji Kata ya Uwemba – Njombe Mjini.

Supplementary Question 1

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, naishukuru sana Serikali kwa mradi huu ambao tumeungojea kwa muda mrefu sana. Ni habari njema sana kwa watu wa Mtaa wa Uwemba. Nina swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu wa maji utategemea chanzo cha maji kinachotoka kwenye milima ya Madope katika Wilaya ya Ludewa. Ili mradi ufanye kazi, ni lazima ni kile chanzo kifanye kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunavyoongea sasa hivi, bomba la kwenda kuunganisha na hicho chanzo lipo tayari, lakini kuna mradi mwingine mkubwa wa barabara ambao umevuruga lile bomba katika baadhi ya maeneo. Sasa swali langu ni je, Serikali inaweza kutoa maelekezo mahususi ili mkandarasi yule ambaye anashughulika na lile bomba au barabara arudishie bomba kwenye maeneo hasa ya Kata ya Luponde maeneo ya Madope ili mradi ule ukikamilika kule maji yaweze kupita? Ahsante.

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba changamoto moja ilikuwa ni fedha, lakini sasa kwa sababu tayari bajeti imeshapitishwa, tumeshaidhinishiwa fedha takribani shilingi trilioni 1.06, sasa zinakwenda kuanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa ni kwamba nataka nitoe maelekezo kwa Meneja wa TANROADS na viongozi wanaohusika na hili, kwa sababu haliwezekani mradi huu ukwame kwa sababu ya ujenzi wa barabara ambao umechukua muda mrefu. Ninawaelekeza na kuwasisitiza na kuwaomba sana wanaosimamia TANROADS, wahakikishe kwamba hili jambo linakwenda kukamilika ili mradi ukamilike na wananchi waweze kupata huduma kwa wakati. Nashukuru. (Makofi)