Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 49 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 635 | 2025-06-19 |
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa Maji Kata ya Uwemba – Njombe Mjini.
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza ununuzi wa kumpata Mkandarasi atakayetekeleza Mradi wa Maji Kijiji cha Uwemba uliopo Njombe Mjini. Kazi zinazotarajiwa kutekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 300,000, ulazaji wa mtandao wa bomba umbali wa kilometa 49.8, na ujenzi wa vituo 12 vya kuchotea maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa mradi huo unatarajia kuanza mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2025/2026 na utakuwa kwa muda wa miezi nane. Nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved