Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini Jeshi la Zimamoto na Uokoaji litakuwa na Ofisi ya kuendesha shughuli zake katika Wilaya ya Nyasa?

Supplementary Question 1

MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nitoe shukrani kwa Serikali kwa kutenga fedha hizo kwa ajili ya kujenga ofisi na maeneo ambayo vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vinafanyia kazi. Ninataka nijue, katika Wilaya ya Mbinga, je, kiasi hiki kilichotengwa kitahusisha na Wilaya ya Mbinga?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Wilaya ya Mbinga ni sehemu ya wilaya zitakazonufaika na mpango huu, na hivyo nikutoe wasiwasi kwamba Wilaya ya Mbinga ni miongoni mwa wilaya ambazo zitapitiwa na mradi huu kwa sababu ni operation ya nchi nzima kuhakikisha Wilaya zote tunazipelekea huduma ya majengo ya zimamoto.

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:- Je, lini Jeshi la Zimamoto na Uokoaji litakuwa na Ofisi ya kuendesha shughuli zake katika Wilaya ya Nyasa?

Supplementary Question 2

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaishukuru Serikali kwa kutuletea Askari wa Zimamoto Wilayani Lushoto, lakini Askari wale walioletwa hawana hata vitendea kazi kama vile gari la zimamoto. Je, lini Serikali itapeleka gari la zimamoto na vitendea kazi vingine ili kuokoa matukio yanapotokea ya moto kwa wananchi wetu?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwamba vifaa vya zimamoto hapa nchini yakiwepo magari vinasambazwa pote nchini. Nilipokuwa nikijibu swali kama hili jana, nilieleza mpango wa Serikali juu ya ununuzi wa vifaa ambavyo vinahusisha magari karibu 100 ambayo yatapokelewa hivi karibuni hapa nchini, na matarajio yetu yatasambazwa katika wilaya zote hapa nchini.