Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali kuokoa maisha ya wananchi kutokana na uwepo wa ajali nyingi katikati ya Mji wa Geita maeneo ya Nyankumbu na Shilabela?

Supplementary Question 1

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali kuhusu elimu inayoendelea kutolewa kwenye maeneo haya ambayo watu wengi wanapoteza maisha nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, je, Serikali imefanya utafiti wa kutosha kujua kwamba ajali hizi zinazotokea inawezekana zikawa zinasababishwa na tatizo la kihandisi (engineering problem)?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa vile pale Nyankumbu kuna soko na vilevile kuna shule, kwa hiyo, wanafunzi wengi wanaopita maeneo hayo na hao wanaoenda sokoni wanagongwa mara kwa mara.

Je, nini mpango wa Serikali kuanza kuweka mazingira ambayo yanaweza kujengwa daraja la juu (fly over) ili kuondoa kabisa tatizo hili la wananchi kugongwa?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Magessa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza suala la usalama barabarani ni suala la wadau wengi; kwanza watumiaji wa barabara, watembea kwa miguu, lakini madereva wa vyombo vya moto, pamoja na Jeshi la Polisi kwa maana ya Kikosi cha Usalama Barabarani. Kwa hiyo, nitoe kwanza wito kwa wale wadau wote hawa kama nilivyojibu jibu la msingi kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuhusu pengine ni tatizo la kiufundi; sote ni mashahidi kwamba barabara zinavyojengwa kwanza unafanyika usanifu wa kina kuhakikisha kwamba inajengwa kwenye viwango, lakini kwa kuwa ajali hiyo imeendelea kutokea, pamoja na kutoa elimu kwa umma lakini pia Serikali itaendelea kufanya utafiti na kuona kama changamoto hiyo inatokana na suala la kiufundi. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba ama tunapunguza au kumaliza kabisa ajali za usalama barabarani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, ujenzi wa daraja la juu; Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi itafanya utafiti na tathmini kuona kama kuna haja ya kujenga daraja la juu. Lengo letu la msingi kama nilivyosema ni kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanaepuka ajali ambazo siyo za lazima ili kuokoa usalama wao waendelee kuwa salama.

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali kuokoa maisha ya wananchi kutokana na uwepo wa ajali nyingi katikati ya Mji wa Geita maeneo ya Nyankumbu na Shilabela?

Supplementary Question 2

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha ya namna ya kukabiliana na majanga yoyote yale yanapotokea na hata ikitokea hawajui nini wafanye, kwa sababu hawana hiyo elimu, lakini hata wanafunzi wetu kuanzia shule za msingi mpaka sekondari hawapati hiyo elimu vya kutosha.

Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba, elimu inatolewa ili kuwaokoa wananchi wetu pale ambapo majanga yanatokea au kuzuia wasikutane na majanga mbalimbali?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecilia Paresso Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitoa elimu hasa kwenye shule za msingi na sekondari juu ya kuchukua tahadhali mbalimbali hasa kwenye masuala ya zimamoto na uokoaji. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali itaendelea kutoa elimu hiyo kuhakikisha kwamba hasa kwenye shule za msingi kule chini kabisa na shule za sekondari ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wetu wanapokua wanakuwa wanaelewa sana kujikinga na ajali mbalimbali au majanga yanavyotokea katika maeneo yetu. Ahsante.