Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 532 2025-06-06

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: -
Je, upi mpango wa Serikali kuokoa maisha ya wananchi kutokana na uwepo wa ajali nyingi katikati ya Mji wa Geita maeneo ya Nyankumbu na Shilabela?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na TANROADS pamoja na Jeshi la Polisi wamekubaliana kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya barabara kwa wananchi na madereva wa vyombo vya moto. Katika eneo la Nyankumbu yamewekwa matuta pamoja na alama ya mwendokasi wa kilometa 50 kwa saa ili kupunguza ajali na kuokoa maisha ya wananchi kwa kuwa eneo hili pamoja na eneo la Shilabela ni maeneo yenye watu wengi na shughuli nyingi za kiuchumi. Aidha, Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji inaendelea na utoaji wa elimu kwa umma juu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga mbalimbali katika mji wa Geita. Ahsante. (Makofi)