Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza: - Je, Serikali imepiga hatua gani katika kurasimisha biashara za sekta isiyo rasmi ili kuongeza uchumi wa nchi?
Supplementary Question 1
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa sekta isiyo rasmi ambayo inabeba wajasiriamali wa aina mbalimbali inakabiliwa na changamoto kubwa ya mitaji ya kifedha. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuzishawishi benki za kibiashara zianzishe madirisha ambayo yatawasaidia hawa watu kupata mikopo ili waweze kuanzisha biashara na kukuza biashara zao?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninaomba nipokee ushauri wa Mheshimiwa Sekiboko. Ushauri wake umechukuliwa na utaenda kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anachokisema Mheshimiwa Profesa Ndakidemi, lakini tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa benki za kibiashara kuwaita watu hao na kuwafuata wajasiriamali wetu kuwapa mafunzo, lakini na kufungua madirisha madogo madogo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu wetu, yaani wajasiriamali wadogowadogo. Kwa hiyo, nikutoe shaka kwamba jambo hilo Serikali imelizingatia na litaenda kufanyiwa kazi. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved