Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 41 | Finance | Wizara ya Fedha | 530 | 2025-06-06 |
Name
Neema Kichiki Lugangira
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza: -
Je, Serikali imepiga hatua gani katika kurasimisha biashara za sekta isiyo rasmi ili kuongeza uchumi wa nchi?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali kupitia TRA ina utaratibu wa kuwatambua walipakodi kulingana na mitaa (Blocks Management System) ambayo husimamiwa na maofisa kodi ambao hutembelea mitaa husika na kufanya ukaguzi kwa wafanyabiashara ili kujua mwenendo wao katika kulipa kodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali kupitia TRA imeendelea kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wadogo wadogo pamoja na kuwapa elimu juu ya huduma za kikodi ikiwa ni pamoja na TIN.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, TRA, TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi na Mifuko ya Kijamii na Wizara ya Viwanda, ipo katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kijiditali kwa wafanyabiashara ndogo ndogo kwa lengo la kuwatambua, kuwawezesha kimitaji na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya biashara zao. Lengo la mkakati huu ni kuwakuza wafanyabiashara na hatimaye kuwaingiza kwenye mfumo rasmi ambao wataweza kusajiliwa na kulipa kodi, ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved