Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, nini mkakati wa kuzijengea uwezo kampuni za ndani kuzipa tender za shilingi bilioni 50 kwani sheria ya manunuzi inaruhusu kupewa tender za shilingi bilioni 20?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza ninaomba nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake. Ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 inazitaka taasisi za Serikali kutenga 30% ya bajeti kwa ajili ya makundi maalum; 10% kwa vijana, asilimia tano kwa wanawake, asilimia tano kwa wazee na 10% kwa watu wenye ulemavu. Je, makundi hayo yana uelewa kiasi gani wa kuzifikia hizo fursa na jinsi ya kupata hizo tender? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwa kuwa kuna wakati Serikali huwa inachelewesha malipo kwa wakandarasi na kusababisha wakandarasi hao kuuziwa dhamana zao katika benki. Je, sasa Serikali haioni umuhimu wa kuwapatia benki guarantee ili hawa wakandarasi wa ndani na wazabuni wasiweze kuuziwa dhamana zao katika benki? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Dkt. Kabati, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujibu maswali hayo, ninaomba nimpongeze sana kwa namna anavyofuatilia taratibu hizi za NeST na 30% iliyowekwa katika makundi maalum. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imetoa 30% kwa makundi maalum wakiwemo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Serikali tayari imetoa maelekezo kwa taasisi zote nunuzi wafuate sheria hiyo ambayo imewekwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uelewa kwa makundi hayo, Serikali kupitia PPRA inaendelea kutoa mafunzo mbalimbali, inaendelea kutoa semina na warsha, kwa mfano, hivi karibuni katika Jiji la Arusha Serikali kupitia PPRA imetoa mafunzo kwa makundi hayo, lakini Mwanza pia imetoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tunavyozungumza katika viunga hivi vya Bunge wapo wataalam wetu wa PPRA katika eneo eletu hili wanatoa maarifa hayo na uelewa. Kwa hiyo, niombe tu Waheshimiwa Wabunge na wenyewe nao wawe mabalozi wa kuelimisha watu wetu katika sehemu mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali lake la pili, ninaomba nimtoe shaka kabisa Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati kwamba Serikali itaendelea kulipa kwa wakati na wale ambao wamechelewa kwa bahati mbaya tu, basi watalipwa na wataendeleza biashara yao kama inavyotarajiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wake tumepokea pia kwamba Serikali iweze kuingilia kati jambo hilo, basi Serikali itafanya hivyo. (Makofi)

Name

Maida Hamad Abdallah

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: - Je, nini mkakati wa kuzijengea uwezo kampuni za ndani kuzipa tender za shilingi bilioni 50 kwani sheria ya manunuzi inaruhusu kupewa tender za shilingi bilioni 20?

Supplementary Question 2

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa benki za kibiashara nchini hutoa mikopo kwa riba kubwa kwa wakandarasi nchini; je, Serikali ina mkakati gani madhubuti na mpango maalumu wa kuwapatia mikopo wakandarasi kwa masharti nafuu? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Maida kwa namna anavyofuatilia unafuu wa wananchi. Serikali tayari imeshatoa maelekezo kwamba wakandarasi wetu hasa wazawa wanapokwenda katika benki zetu za kibiashara wapewe mikopo kwanza stahiki lakini na kwa riba nafuu. (Makofi)