Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 41 | Finance | Wizara ya Fedha | 529 | 2025-06-06 |
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: -
Je, nini mkakati wa kuzijengea uwezo kampuni za ndani kuzipa tender za shilingi bilioni 50 kwani sheria ya manunuzi inaruhusu kupewa tender za shilingi bilioni 20?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kifungu cha 57 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Namba 10 ya Mwaka 2023 na kanuni ya 45 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za Mwaka 2024 zimetenga zabuni za hadi shilingi bilioni 50 kwa ajili ya wazawa na kampuni za ndani. Utekelezaji wa sharti hili la sheria linatekelezwa kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST).
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kifungu cha 61 cha sheria hiyo, kinaelekeza watu au kampuni binafsi kama hazina uwezo wa kutekeleza mikataba kuingia katika ushirika kwa lengo la kuimarisha uwezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mfumo wa NeST, kuna kategoria mbalimbali za wazabuni ambapo kampuni itatambuliwa na Mfumo wa NeST kama kampuni ya ndani endapo kampuni hiyo imesajiliwa Tanzania; inamilikiwa na raia wa Tanzania kwa 100% au raia wa Tanzania anamiliki mtaji wa hisa katika kampuni hiyo zisizopungua 51%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa timu ya ujenzi wa Mfumo wa NeST inakamilisha ujenzi ndani ya mfumo wa namna ya kutekeleza masuala ya upendeleo kwa wazawa. Hivyo, utekelezaji wa sharti la upendeleo kwa wazawa ndani ya Mfumo wa NeST linatarajiwa kuanza Julai, 2025. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved