Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itatatua tatizo la kukosa huduma ya umeme katika Vitongoji vya Jimbo la Tabora Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Kwa kuwa bado malalamiko mengi kwamba umeme unavyopelekwa kwenye vitongoji, majengo ya kutolea huduma kama hospitali, shule, na miradi ya maji, bado inakuwa hayajapelekewa umeme, je, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba umeme unapofika kwenye kitongoji moja kwa moja unafika kwenye majengo ya kutolea huduma?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa Serikali imefanya kazi nzuri ya kupeleka umeme kwenye vijiji na vitongoji katika maeneo yetu, je, ni upi mkakati wa kuhakikisha kwamba ile bei ya kuingiza umeme ya shilingi 27,000.00 inarejeshwa katika maeneo mengi ili kuwapa wananchi nafuu?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli yamekuwepo malalamiko kwamba, baadhi ya maeneo yenye huduma muhimu huwa yanasahaulika kupelekewa umeme wakati umeme unapopelekwa vijijini.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wote Serikali imesisitiza kwamba kipindi kile ambapo survey zinafanyika, ni vizuri viongozi wa maeneo yale wakahusika, wakashirikiana na wakandarasi kuyabaini maeneo yale ili yaweze kuingizwa kwenye maeneo ambayo yatahakikishiwa yatapata umeme wakati huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili linaposhindikana kufanyika, matokeo yake tunakuta tunapata hii changamoto. Kwa hiyo, rai yangu ni kwa viongozi kwenye maeneo yetu, wawe makini wakati ule wahandisi wanapokuja kufanya survey, basi waweze kushiriki ili kuainisha maeneo muhimu yasijeyakaachwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na hili la bei, kama tulivyosema tangu awali, msingi wa bei hii ni kutambua maeneo kwa mujibu wa taratibu zetu za Kiserikali yanayoainishwa kwamba ni maeneo ya vijijini. Pale ambapo maeneo hayo kwa bahati mbaya yamesahaulika, Serikali tupo tayari kupokea ushauri kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge na mamlaka zilizopo kule kwenye halmashauri ili maeneo haya yaweze kuingizwa kwenye utaratibu wa kulipa bei hii ya shilingi 27,000.00.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved