Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Martha Festo Mariki
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini tatizo la maji litamalizwa kwa maeneo yasiyo na mito, mabwawa au mradi wa maji ya Ziwa Victoria hasa Kijiji cha Kiomboi, Kitongoji cha Madole Sita?
Supplementary Question 1
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wetu wa Katavi una changamoto ya maji kutokana na kuwa na wimbi kubwa la wageni wanaokuja kutafuta fursa mbalimbali za kibiashara. Je, upi mkakati wa Serikali sasa kutoa maji katika Ziwa Tanganyika na kuyaleta katika Mji wa Mpanda ili wananchi wetu waweze kupata maji ya uhakika? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, tayari Serikali kwa kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge wa Mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa tumeshaanza kufanya survey ili kuhakikisha tunahitaji fedha kiasi gani, lakini pia kuna maeneo mengine ambayo tayari wameshaanza kutumia maji ya Ziwa Tanganyika. Kwa upande wa Katavi bado hatujaanza kutumia maji hayo, lakini kuna miradi mikubwa inaendelea katika Mji wa Mpanda na kuna Mradi wa Miji 28 unaendelea, ambapo ukishakamilika upatikanaji wa maji ni zaidi ya 80%, kwa upande wa Mpanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge na Serikali itaendelea kuharakisha kufanya feasibility study and details design, ili kuhakikisha tuna-establish gharama ambazo zitahitajika kwenda kujenga mradi huo na wananchi waanze kufaidika na maji ya kutoka Ziwa Tanganyika, hasa Mkoa wa Rukwa, Katavi na Kigoma, ahsante sana.
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini tatizo la maji litamalizwa kwa maeneo yasiyo na mito, mabwawa au mradi wa maji ya Ziwa Victoria hasa Kijiji cha Kiomboi, Kitongoji cha Madole Sita?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri kuwa katika taasisi za elimu, hasa shule za sekondari na msingi, hazina maji ya uhakika. Aidha, kutokana na wakati mwingine bili kuwa kubwa wanashindwa kulipa.
Je, hawaoni kwamba, ni muda muafaka sasa kuwachimbia visima katika maeneo hayo, hasa zile shule ambazo zinasuasua katika ulipaji wa bili, ili wawe na maji ya uhakika? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, ni lengo la Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba Watanzania wanaweza kuwa na accessibility ya maji, na maji hayo yawe affordable, safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo ambayo tutachimba visima pale ambapo tukipima na kujiridhisha maji chini ya ardhi yanapatikana na pale ambapo tutajiridhisha maji chini ya ardhi hayapatikani, tutafanya extension ya miradi iliyopo pale karibu. Gharama hazitakwepeka kwa baadhi ya maeneo, lakini kuna maeneo ambapo tutakapoweza kuchimba visima tunaweza kukwepa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika usanifu wa miradi mikubwa tumeendelea kutoa kipaumbele kwenye taasisi za umma; zahanati, vituo vya afya na pia shule za msingi na sekondori. Lengo ni kuhakikisha kwamba watoto wetu wanapokuwepa shuleni wawe na uhakika wa kupata huduma ya maji safi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama kubwa za maji zitasababisha baadhi ya shule kushindwa kulipia na ukishindwa kulipia matatizo yatarudi kwa watoto wetu ambao wapo katika shule hizo. Tunapokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge wa Ilemela, mahiri kabisa, tutaendelea kuufanyia kazi na kuchakata kuona ni kwa namna gani tunashirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kuja na mkakati mzuri zaidi wa kutatua changamoto hii kwa muda ambao unakuja, ahsante sana.
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini tatizo la maji litamalizwa kwa maeneo yasiyo na mito, mabwawa au mradi wa maji ya Ziwa Victoria hasa Kijiji cha Kiomboi, Kitongoji cha Madole Sita?
Supplementary Question 3
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwa kuwa maeneo mengi kuna ukame na kuna uhitaji mkubwa sana wa mabwawa kama Kiteto. Nini mpango wa Serikali kutafuta pesa maalum kwa ajili ya kujenga mabwawa Kiteto?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninamshukuru sana Mheshimiwa Olelekaita, Mbunge wa Kiteto kwa kuendelea kuwa mshauri mzuri katika sekta yetu ya maji pale ambapo tutakuwa tunahitaji, lakini pia kwa kuendelea kutoa maoni ya namna gani tunaweza tukaboresha zaidi katika kutatua huduma ya maji nchini, hasa katika maeneo yenye ukame. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimesema hapo awali Serikali tayari imeshaanza kujenga mabwawa mengi tu ya kutosha katika maeneo ambayo yana ukame na tunafahamu kwamba maendeleo ni hatua kwa hatua. Kama ambavyo tumeshakamilisha mabwawa 45 na mabwawa 19 yakiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji, tunaendelea kufanya tathmini pale ambapo yanakuwa yamebaki tunahitaji kiasi fulani, ili tuweze kuweka mkakati maalum wa kupata hizo fedha kwa ajili ya mabwawa ambayo yataenda kutosheleza katika maeneo mengi yenye ukame.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile mabwawa peke yake hayatakuwa suluhisho la kudumu katika baadhi ya maeneo, na ndiyo maana maeneo kama ya Tabora, ilionekana kabisa upatikanaji wa maji chini ya ardhi ulikuwa ni tatizo kubwa. Ndio maana Serikali ikaweka shilingi bilioni 680 ikafikisha pale, ikaweka shilingi bilioni 143 Sikonge, Kaliua na Urambo, lakini pia imeendelea kufanya extension Igunga shilingi bilioni 22. Mambo haya yanafanyika kwa sababu Serikali ina dhamira ya dhati kabisa ya kuhakikisha kwamba wananchi wake, haijalishi wapo katika maeneo gani, wanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza. Mheshimiwa Mbunge tumepokea ushauri wako tutaufanyia kazi, ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved