Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Water and Irrigation Wizara ya Maji 524 2025-06-06

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARTHA F. MARIKI K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: -

Je, lini tatizo la maji litamalizwa kwa maeneo yasiyo na mito, mabwawa au mradi wa maji ya Ziwa Victoria hasa Kijiji cha Kiomboi, Kitongoji cha Madole Sita?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote vinafikiwa na huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali inatekeleza programu ya uchimbaji wa visima vitano kwenye kila jimbo, hususan kwenye vijiji visivyokuwa na huduma ya maji nchini. Kupitia programu hiyo Kitongoji cha Madole Sita kilichopo Kijiji cha Kiomboi, Wilayani Sikonge kitachimbiwa kisima kirefu, kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa eneo hilo ambapo kwa sasa kazi ya utafiti wa maji chini ya ardhi inaendelea. Aidha, Serikali inaendelea na mradi wa utafiti wa maji ardhini na uchimbaji wa visima 17 katika vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji Wilayani Sikonge.