Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 1

MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.

Je, ni lini Serikali itakuwa na mpango maalum wa kubadilisha mita za zamani na kufunga mita za malipo kabla ya matumizi kwenye miradi yote ya zamani ili kuboresha malipo na kurahisisha kwa zile jumuiya za maji?

Swali la pili, mradi huu wa maji wa Kata ya Kalulu ulikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu toka mwaka 2017, huu ni muda mrefu sana mpaka sasa ule mradi haujakamilika.

Je, Waziri anakauli gani ya kuwambia wananchi wa Kalulu kwamba mradi ule utakamilika kwa wakati ili kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Waziri na kumtua Mama ndoo kichwani? Ahsante. (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na pia ninamshukuru Kaka yangu Mheshimiwa Hassan Zidadu Kungu, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, kwa kazi kubwa na nzuri ambayo anaendelea kuifanya na kuwatetea wananchi wake na hakika pia kuungana na Mheshimiwa Rais kwenye ajenda yake ya kumtua mama ndoo kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele cha kwanza, kufunga prepaid water meter, tayari Wizara ya Maji imeshaanza kufunga prepaid water meter kulingana na wateja wapya, kwa sababu hizi ni gharama ambazo zinabebwa na Serikali moja kwa moja, kwa hiyo, tunachofanya ni kwamba, wale wapya tunaanza kuwafungia wanapoomba yale maombi ya kuunganishiwa maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kwamba tutaenda sasa kuanza ku-phase out zile mechanical meters ambazo zilikuwepo hapo kabla, ambazo zilikuwa zinatumika hatua kwa hatua kulingana na fedha ambazo zitakuwa zinapatikana. Lengo kubwa la kufunga prepaid water meter tunaamini kwamba kwanza kabisa itapunguza changamoto za bili ambazo zinakuwa zinaleta utata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na predictable mapato ya hizi jamii zinazohudumia maji (CBWSO) na hata mamlaka zingine. Lengo ni kwamba tuhakikishe hatuna malalamiko na mwananchi aweze kujipangia namna gani atumie maji yake. Tunaendelea kulifanyia kazi kulingana na kwamba linahitaji fedha na tutaenda hatua kwa hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ya mwaka 2017; imekuwa ni kawaida kwa Serikali kuendelea kuchukua hatua mbalimbali kutekeleza ahadi ambazo zimetolewa na viongozi wetu wa kitaifa akiwemo Mheshimiwa Rais mwenyewe, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, na Naibu Waziri Mkuu. Lengo ni kwamba tunapokuwa tunatekeleza ahadi hizi ni kujenga imani ndani ya Serikali lakini pia ni kuwajengea imani Watanzania juu ya viongozi wao wa kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hili suala la Tunduru Kaskazini tumeshalichukua na Mheshimiwa Mbunge alishatueleza mara kadhaa kuhusiana na hili suala. Nikuhakikishie kwamba sasa tunaenda kulifanyia kazi, lakini kipengele cha fedha kitakuwa kinahusika sana ili kuhakikisha kwamba utekelezaji wake unakuwa wa ukamilifu zaidi, ahsante sana. (Makofi)

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Rungwe, Mji wa Tukuyu ni mji ambao ni sehemu ambayo inanyesha sana mvua lakini tunapata sana shida ya maji. Ni lini Serikali mtawekeza nguvu katika mji huu wa Tukuyu ili wananchi hawa waweze kupata maji kwa sababu wametoka Nyanda za Juu Kusini sehemu zenye mvua nyingi, lakini shida ni kubwa sana ya maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, hakika wakina mama wanaendelea kuonesha juhudi zao za kuwatetea akina mama wenzao katika kumtua mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali ni kuendelea kuhakikisha kwamba maji juu ya ardhi yanayotokana na mvua, tunajenga mabwawa kama ambavyo sasa tayari tumeshajenga mabwawa 45 na kuna mabwawa takribani 19 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Lengo ni kuhakikisha kwamba tunakuwa tunatengeneza catchment ya maji yasipotee wakati tunajua kabisa kwamba katika maeneo fulani hayana vyanzo vya uhakika vya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sisi kama Serikali tumeshaweka mpango huo, pale ambapo hakuna mito, pale ambapo hakuna ziwa, pale ambapo maji chini ya ardhi ni tatizo tunatumia maji ya mvua na kwa kuyatengenezea mabwawa ili tuweze kuyatumia kwa ajili ya kusambaza maji safi na salama kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tuko na yeye na yeye tunamuomba kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili kuhakikisha kwamba tunafikisha huduma ya maji safi na salama, ahsante sana. (Makofi)

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 3

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa nafasi ya kuuliza swali. Ninaipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetujengea mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria kwa kuhudumia Kata za Kashenye na Kanyigo kwa awamu ya kwanza na baadaye awamu ya pili Kata ya Gwanje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo sasa hivi ni takribani mwaka mmoja tangu umefika hatua ya utekelezaji ya 92%; sasa ni nini kauli ya Serikali kuhakikisha mradi huo unakamilika sasa na unawatua wananchi wa Wilaya ya Missenyi katika Kata za Kanyigo na Kashenye ndoo kichwani ili waweze kupata huduma ya maji? Ahsante.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Serikali pia ninapokea pongezi za Mheshimiwa Kyombo, hakika anaendelea kutupatia ushirikiano mzuri na ndio maana anajua hata progress ya mradi umefikia asilimia ngapi kwa sababu amekuwa karibu sana na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mradi huo ni uwekezaji mkubwa sana wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na ametoa fedha nyingi na ndio maana na sisi tunaendelea kuusukuma ili ukamilike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tunachokihitaji hata kabla ya mradi haujakamilika kuna existing infrastructure ambazo zina uwezo wa kupokea maji kabla ya mtandao mpya haujakamilika. Ninawaelekeza Kagera ili waweze kuangalia namna bora zaidi ya kuanza kutoa huduma ya maji wakati mradi ukiwa unaendelea kukamilika. Nimtoe hofu hilo wataalam wetu watalifanyia utafiti mzuri ili tuweze kufikisha huduma ya maji safi na salama, ahsante sana.

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 4

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana, kule Halmashauri ya Mji Njombe tuna mradi mkubwa wa maji unaitwa Igongwi ambao una-supply kata tatu. Mradi huu tunamshukuru Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Waziri, kwa kuwa umekamilika kwa 97% lakini chanzo cha maji kinatoka Ludewa na maji yanapita kijiji kinaitwa Luvuyo na wananchi wa Luvuyo wamezuia mradi huu usikamilike kwa kuruhusu maji yapite kwenye kijiji chao mpaka wao wapate maji.

Nini kauli ya Serikali kuhusiana na kuwasaidia wananchi wa Luvuyo ili wananchi hawa wa kata zile tatu na wenyewe wapate maji? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na pia ninamshukuru sana Mheshimiwa Mwanyika, Mbunge wa Njombe na naomba kumjibu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni sera ya sekta ya maji pale ambapo mradi mkubwa unapita, kushoto kulia kilometa 13 wahusika wanaoishi katika maeneo hayo ni lazima wapate huduma ya maji safi na salama, hilo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, pale kwenye chanzo ambapo tunachukua maji, wananchi wanaoishi katika maeneo ya vyanzo ni lazima wawe kipaumbele kupata huduma ya maji safi na salama. Tunatambua kwamba hata usanifu wetu tunapofanya usanifu wa miradi tunahakikisha kwamba mazingira kama hayo yanakuwa sehemu ya usanifu wetu ili kutoleta changamoto nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunatambua katika mradi huu, katika eneo la Luvuyo ambayo kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema, pale kinachoendelea sasa hivi tulishatoa maelekezo kwa RM Mkoa wa Njombe kufanya majadiliano ya kina ili kuhakikisha kwamba wananchi wanaopitiwa na mradi huo wanapata huduma ya maji safi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, ninatoa maelekezo kwa RM Njombe kuharakisha hayo majadiliano ili kuhakikisha sasa tufikie mwisho na hatua zichukuliwe na wananchi wanaopitiwa na mradi huo wapate huduma ya maji safi na salama.

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 5

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Waziri, sisi tushukuru Mji wa Babati upatikanaji wa maji sasa ni 98% lakini tatizo letu ni bili kubwa ya maji. Wananchi wa Babati wanalipa zaidi ya shilingi 1,800 kwa unit moja na ninadhani maeneo mengine nchini ni kama 300 au 700. Ni nini kauli ya Serikali juu ya kupunguza bili hizi za maji katika Mji wa Babati kwa sababu wananchi wanashindwa kuzilipia? Ahsante. (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Gekul kwa kuendelea kuwapambania Wana-Babati. Ni kweli kabisa gharama za maji inategemea na gharama za uzalishaji na uzalishaji inategemea kwamba ni njia gani iliyotumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ni maji tunayapata kwa njia ya mserereko basi gharama yake itakuwa tofauti, tukipata maji kwa njia ya kutumia umeme wa solar maana yake gharama yenyewe pia itakuwa tofauti, lakini tukipata kupitia umeme wa Gridi ya Taifa gharama yake itakuwa tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, gharama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine inatofautiana kulingana na aina ya uzalishaji. Hata hivyo, uchangiaji wa maji ni suala ambalo hatuwezi kulikwepa iwapo tutazuia au tutapunguza sana gharama za uchangiaji wa maji, maana yake kwamba sustainability ya miradi hiyo itafikia kipindi watashindwa ku-repair hata vitu vidogo vidogo vitakapokuwa vinaharibika na matokeo yake mradi mzima utakuwa na changamoto ambayo hawataiweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge, tunalipokea kama Serikali. Tutatuma wataalamu wetu waende kufanya tathmini na kuangalia gharama za uzalishaji na gharama ambayo tunaifikisha kwa mtumiaji ili tuone kama kuna nafasi ya kupunguza. Serikali haitasita kuchukua hatua ya kupunguza gharama ili mradi Mtanzania apate maji kwa gharama ambayo inakubalika, ahsante sana.

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 6

MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kuniona. Ninaipongeza sana Serikali kwa kazi kubwa iliyofanyika Buchosa kwenye upande wa maji. Kuna kiasi cha shilingi bilioni 21 zipo kwenye miradi ya maji tayari, lakini ipo changamoto moja kubwa watu wetu Buchosa wanaliwa sana na mamba na maeneo ya Kanda ya Ziwa miradi hii haijafika.

Je, Serikali iko tayari kuongeza GP kwenye maeneo kama Maisome, Kanyala, Nyakalilo ili watu waweze kujipatia maji kwa urahisi na kuweza kuokoa maisha yao? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Eric Shigongo, Mbunge wa Buchosa kwa kuendelea kuwasemea wananchi ili kuwaondosha katika hatari ambayo mamba kwa kweli ni Wanyama wakali na wanaweza wakasababisha majanga makubwa na Serikali isingependa kuwaweka wananchi wake katika mazingira ambayo hayana usalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni ombi la Mheshimiwa Mbunge na sasa Serikali tunalipokea ombi hili na tutatuma wataalam wetu kwenda kuangalia namna bora zaidi ya kuchukua hatua stahiki ili kuepusha mazingira hatarishi kwa wananchi wetu, lakini pia waweze kupata huduma ya maji safi na salama. Mheshimiwa Mbunge, Serikali tutaenda kulifanyia kazi kwa uzito stahiki. (Makofi)

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 7

MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, mkandarasi anayejenga mradi wa maji katika Vijiji vya Tandali, Homboza na Mlali amekuwa akisuasua sana kwa kisingizio cha kutokulipwa kwa wakati na mpaka sasa yupo chini ya 60%. Je, nini kauli ya Serikali juu ya kumlipa huyu mkandarasi ili aweze kumalizia miradi hii mikubwa ya maji katika vijiji nilivyovitaja? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Jonas, Mbunge wa Mvomero, kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakumbuka nilifika Mvomero tukapita katika maeneo na upatikanaji wa maji Mvomero kwa kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan umeongezeka kwa kasi kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado tunatambua kwamba bado kuna changamoto za hapa na pale, lakini pia tunatambua kwamba wakandarasi wetu wanahitaji fedha ili waweze kuendelea na miradi. Tayari Waziri wa Maji, amemuelekeza Katibu Mkuu ili waweze kukusanya maombi yote zile hati za madai ili wakandarasi walipwe na waendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna majadiliano na wenzetu Wizara ya Fedha kuendelea kuhakikisha kwamba upatikanaji wa fedha unaendelea kuwepo ili na sisi Wizara ya Maji, tuweze kuwalipa wakandarasi wetu na waendelee na kazi. Nikutoe hofu tutaendelea kulifanyia kazi. (Makofi)

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 8

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana, wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, ndani ya jimbo langu pamoja na shughuli zingine ulizindua mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Michiga ambapo Vijiji vya Michiga, Mnazimmoja na Pachani vitanufaika na mradi huo.

Kwa kuwa mradi ulizinduliwa bila kukamilika kwa 100%; je, Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba mkandarasi yule anakamilisha mradi ule kwa wakati ili wananchi wa vijiji husika wakanufaika na mradi huo? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Yahya Mhata kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Serikali hairuhusu mradi kuzinduliwa ukiwa haujakamilika kwa 100%, lakini kama kukiwa kuna mazingira ya kuuzindua basi tumeshajiridhisha kwamba, kwanza; kutakuwa na ubora wa maji unaotakiwa na pili; kutakuwa na mazingira ya miundombinu kuwa yamekamilika bila kusababisha upotevu wa maji iwapo yataanza kutumika. Kwa mantiki hiyo na kwa muktadha huo mradi kama umefikia asilimia nzuri kabisa nimtoe hofu, Serikali tupo tayari kumsisitiza mkandarasi akamalizie vipengele ambavyo vinaonekana havijakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, japo kwa sasa sina taarifa sahihi, lakini ngoja nikitoka hapa nitaenda kulifanyia kazi na nitampa mrejesho Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kuona namna gani unakamilika kwa 100%. (Makofi)

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 9

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, hivi karibuni tumeona miradi mikubwa sana ya maji mbali kutoka katika vyanzo vya maji kama Ziwa Victoria na Lake Tanganyika, lakini maeneo ambayo yapo karibu na maziwa au vyanzo hivyo hayana maji.

Je, ni lini Serikali sasa itabadilisha sera hiyo ili maeneo ambayo yapo karibu na hivi vyanzo vya maji yapate maji? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Kajege na yeye anatoka Kanda ya Ziwa yupo karibu na Ziwa Victoria, ninaamini kabisa kwamba anatamani pia kwamba maji yaweze kumfikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sera ya Serikali ni kuhakikisha kwamba vyanzo vyetu vya uhakika ni maziwa, mito na mara nyingine tunachimba, lakini na maji chini ya ardhi kwa kuchimba visima. Kwa sasa Serikali iliwekeza uwekezaji mkubwa sana kwa Ziwa Victoria na ndio maana maji yakafika Tabora kwa shilingi bilioni 680.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali kupitia mradi wa mabadiliko ya tabianchi ambapo tunayachukua maji Ziwa Victoria kupeleka Nyanshimo, Bariadi, Itilima, Maswa pamoja na Meatu, huo ni mkakati wa Serikali kuendelea kuwekeza, lakini pia sasa tunafanya feasibility study and details design kwa ajili ya matumizi ya Ziwa Tanganyika kwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Lengo ni kwamba tunaenda kutumia vyanzo vyetu vya uhakika, mito mikubwa kama Malagarasi na maziwa mengine yote ili tuweze kuyatumia kwa manufaa ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimtoe hofu, mkakati na sera ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tunatumia vyanzo hivyo lakini kwa mazingira ambayo yanaruhusiwa. (Makofi)

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 10

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru na ninaishukuru Serikali kwa kupeleka shilingi milioni 240 Kijiji cha Unyari kumalizia kazi na kumalizia lambo la Mihingo. Wiki mbili zilizopita Mheshimiwa Waziri wa Maji aliagiza mitambo iende Kijiji cha Mkomariro na Kijiji cha Kyandege kuziba lambo la Kyandege na lambo la Mkomariro, sasa mpaka leo ni wiki ya tano hiyo mitambo haijaenda; je, lini mitambo hiyo itaenda?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapokea changamoto hii kutoka kwa Mheshimiwa Getere na kuona namna gani Waziri wa Maji ameagiza na halijatekelezwa. Ninatoka hapa kwenda kufuatilia utekelezaji wake wa maelekezo ya Waziri wa Maji, ahsante sana. (Makofi)

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 11

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Gitting ilikuwa inategemea maji kutoka vyanzo vya Mlima Hanang. Baada ya maporomoko ya mlima, upungufu wa maji umekuwa mkubwa sana, lakini survey imeshafanyika kuchimba visima viwili. Je, lini visima hivyo vitachimbwa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana Mheshimiwa Engineer Samweli, ninakumbuka pia tuliweza kutembelea katika maporomoko yale ya Hanang na tuliona namna gani miundombinu ilivyokuwa imeharibiwa, lakini Serikali iliwekeza fedha pale kurejesha ile miundombinu pamoja na kutengeneza njia mbadala ya kupata huduma ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hivi visima viwili ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja, ninaomba nivipokee kwa ajili ya ufuatiliaji tuone kwamba vinaweza kuanza kuchimbwa lini, lakini ninatambua kwamba Wizara ya Maji kupitia bajeti yake ambayo tumeipitisha 2025/2026 inaenda kutatua changamoto ya maeneo ambayo hayana maji kutokana na miradi mikubwa kutopita sasa tunaenda kuchimba visima katika vijiji vingi ambavyo vitakuwa havijapitiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu na hivi vijiji viwili vitakuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huo wa uchimbaji wa visima.

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Supplementary Question 12

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninataka kufahamu ni upi mkakati walionao kama Wizara kuongeza flow ya maji katika Mji wa Isongole kwani maji yapo, lakini kwenye bomba yanatoka kidogo sana?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama flow ya maji ni ndogo maana yake pressure yake siyo nzuri na kama pressure yake sio nzuri kuna mambo mawili yanaweza yakatokea pale. Inawezekana jiografia ya pale inasababisha kuna maeneo mengine maji yanafika yakiwa pressure imeshakuwa ndogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaagiza wataalam wetu wakafanye utafiti pale, wajiridhishe kama tutahitaji kuweka booster station katikati ili kuongeza speed ya maji kuwafikia wateja basi tutafanya hivyo, lakini kama kutakuwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ambapo kuna upotevu wa maji sehemu fulani inatokea basi napo tutachukua hatua stahiki kuhakikisha kwamba maji hayapotei yanafika kwa wateja yakiwa na kasi inayotakiwa kwa ajili ya wananchi kuyatumia, ahsante sana.