Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Water and Irrigation Wizara ya Maji 523 2025-06-06

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa maji katika Kata ya Kalulu ili kumtua mama ndoo kichwani na kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 itaanza utekelezaji wa mradi wa maji wa Kata ya Kalulu uliopo Wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma. Kazi zinazotarajiwa kutekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa nyumba mbili za mitambo (pump house), ufungaji wa pampu za kusukuma maji, ujenzi wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 50,000 kila moja, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 13, sanjari na ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji vya malipo ya kabla. Mradi huo unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 4,715 waishio katika vijiji viwili vya Rahaleo na Mbungulaji vilivyopo katika Kata ya Kalulu.