Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: - Je, kwa nini Pensheni hazibadiliki na kupanda kutokana na mfumuko wa bei?
Supplementary Question 1
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Labda kwa maslahi ya wastaafu, kwenye bajeti ya 2026 pensheni hii imepandishwa zaidi kutoka shilingi 150,000.00 inafika mpaka shilingi 225,000.00 tulivyoelezwa jana. Nina maswali mawili ya nyongeza: -
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza. Katika Mji wa Iringa tulikuwa tuna watendaji 25 waliokuwa wamejitolea na walipewa kibali cha kuajiriwa, lakini baadaye Katibu Mkuu aka-stop kwamba tusubiri, atatoa tena maelekezo mapya, mpaka leo hawajaajiriwa tangu mwaka 2024. Ni lini Serikali itawaajiri watendaji hawa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kuna mwalimu wetu mmoja wa kike anaitwa Rachel anayejitolea katika shule yetu ambayo iko mbali sana, na ni shule ambayo haina mwalimu wa kike kabisa. Huyu mwalimu amekuwa anafanya interview muda wote, kosa lake ni kwamba yeye ana Degree, lakini walimu waliokuwa wanachukuliwa ni wenye Diploma, naye alikuwa tayari kujitolea, na amejitolea zaidi ya miaka nane katika shule hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali haioni kwamba inaweza kuwafanyia consideration ili aajiriwe moja kwa moja, kwa sababu shule hiyo iko katika mazingira ya mbali ambayo walimu wa kike wanashindwa kwenda kufundisha kule?
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Moja, walimu wa kujitolea, kama utakumbuka vizuri, Waziri wa Utumishi alilitolea maelekezo na namna atakavyolifanyia kazi kwa wale watumishi wote ambao wanajitolea katika maeneo mbalimbali. Naomba tuendelee kuwa wavumilivu wakati Serikali inalifanyia kazi, kwa sababu ya uhalisia juu ya hawa watu ambao wanajitolea na kutoa michango mingi kwa Serikali yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili kuhusu nyongeza, I mean binti anayejitolea katika shule mojawapo katika mkoa wa Mheshimiwa Mbunge, hebu tulichukue, tutawafikishia watu wa Wizara ya Utumishi ili tuone namna nzuri ya kumsaidia binti huyu. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved