Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 49 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 626 2025-06-19

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: -

Je, kwa nini Pensheni hazibadiliki na kupanda kutokana na mfumuko wa bei?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kupanda kwa pensheni hutegemea hali ya uhimilivu wa mifuko. Serikali hufanya tathmini ambayo matokeo ya tathmini hizo huwezesha kujua mifuko kama ni himilivu na ina uwezo wa kuhuisha pensheni za wastaafu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuboresha mafao, Serikali kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imepandisha kiwango cha Pensheni kutoka shilingi 100,000.00 hadi kufikia shilingi 150,000.00 kwa mwezi, kuanzia mwezi Januari, 2025, na pia kuhuisha pensheni kwa wastani wa asilimia mbili kwa kuzingatia mfumuko wa bei. Serikali itaendelea kuhuisha pensheni kadri uhimilivu wa mifuko yetu unavyoendelea kuimarika.