Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Kasalali Emmanuel Mageni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sumve
Primary Question
MHE. KASALALI E. MAGENI K.n.y. MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Shule za Sekondari Bulamba na Nansimo ili zitoe elimu ya kidato cha tano na sita?
Supplementary Question 1
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri kwa niaba ya watu wa Mwibara, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Shilanona katika Jimbo la Sumve kimeanza ujenzi wa shule ya sekondari ambayo mpaka sasa Mfuko wa Jimbo na wananchi tumeshatumia zaidi ya shiingi milioni 70 na shule ile bado haijaisha.
Je, ni lini Serikali itatupatia pesa kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa shule ile ili watoto wa Shilanona ambao wanatembea umbali mrefu kwenda Shule ya Sekondari Wala, waweze kupata huduma ya sekondari karibu?
Swali la pili, Shule ya Sekondari ya Wala ni shule ambayo ina wanafunzi wengi sana, na imefika hadhi ya kuwa na kidato cha tano na sita. Je, ni lini Serikali itaongeza majengo na kuipandisha hadhi shule hiyo iwe ya kidato cha tano na cha sita?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza ninawapongeza sana wananchi wa Jimbo la Sumve pamoja na Mheshimiwa Mbunge Kasalali Mageni, kwanza kwa wananchi kuchangisha michango yao kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule hii ya sekondari kwa kidato cha kwanza hadi cha nne, lakini pia Mheshimiwa Mbunge kupeleka fedha pale za Mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, kwa sababu umeshawasilisha hoja hiyo Serikalini na Serikali hii sikivu inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tumeshachukua hoja ya wananchi wa Sumve, tumeshaiweka kwenye Mpango wa SEQUIP kwa ajili ya kupeleka fedha ili tuweze kuikamilisha Shule hiyo ya Sekondari ya Shilanona. Kwa hiyo, ninaomba tu nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Sumve kwamba Serikali inalifanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, zipo shule nyingi ambazo zina sifa ya kuwa kidato cha tano na cha sita ikiwemo shule ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja kwa idadi ya wananchi pia kwa uhitaji wenyewe wa shule ya kidato cha tano na sita, nikuhakikishie tu kwamba, kupitia mpango wa SEQUIP tumeainisha maeneo yote ya kipaumbele kwa ajili ya kuanza kujenga shule za kidato cha tano na sita na tutatoa kipaumbele katika shule hiyo ili iweze kujengwa.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. KASALALI E. MAGENI K.n.y. MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Shule za Sekondari Bulamba na Nansimo ili zitoe elimu ya kidato cha tano na sita?
Supplementary Question 2
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, katika Jimbo la Tarime Vijijini unakuta kuna shule moja ina walimu watatu wa Kiswahili, lakini shule jirani haina Mwalimu wa Kiswahili, halafu shule nyingine ina walimu wawili wa hesabu, lakini shule nyingine haina mwalimu wa hesabu, hivyo hivyo katika masomo mengine.
Je, Serikali ipo tayari kutoa mwongozo na maelekezo mahsusi pale Tarime Vijijini ili wafanye msawazo, palipo na upungufu wa walimu kwa masomo fulani walimu wapelekwe ili wanafunzi wote kwa pamoja waweze kupata elimu inayofanana na wafanye mitihani sawasawa, ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali ilishatoa mwongozo, kwanza kuhakikisha kwamba shule katika halmashauri na mikoa yetu zinakuwa na usawa katika upatikanaji wa walimu wa masomo mbalimbali wakiwemo walimu wa masomo ya hisabati na masomo ya sayansi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi hii kwa sababu ni wajibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime, ni wajibu wa Afisa Elimu Sekondari na Msingi wa Halmashauri ya Tarime, pia ni wajibu wa REO - Afisa Elimu wa Mkoa wa Mara. Nitoe maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kwamba ndani ya wiki mbili wapitie shule hizo ambazo zina walimu wengi zaidi wa hisabati na sayansi na waangalie zile shule ambazo zina walimu wachache zaidi ili wafanye msawazo wa ndani wa kuhamisha walimu kwenda kwenye shule ambazo hazina walimu kabisa, wakati Serikali ikiendelea kuandaa vibali kwa ajili ya kwenda kuziba gap la watumishi katika maeneo hayo. (Makofi)
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. KASALALI E. MAGENI K.n.y. MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Shule za Sekondari Bulamba na Nansimo ili zitoe elimu ya kidato cha tano na sita?
Supplementary Question 3
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi, Kata ya Nzihi katika Jimbo la Kalenga ina shule za sekondari mbili, lakini watoto wanakwenda mbali sana kutafuta masomo ya kidato cha tano na cha sita; je, ni mpango gani wa Serikali kutupatia shule ya kidato cha tano na cha sita?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya vipaumbele vya Serikali ni kuhakikisha tunasogeza huduma za elimu karibu zaidi na jamii na wanafunzi ili kuepuka wanafunzi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kidato cha tano na sita.
Kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi hii kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Kiswaga kwamba Serikali kupitia mpango wa SEQUIP imeendelea kuainisha maeneo yenye uhitaji wa shule za kidato cha tano na sita, tutaipitia pia Kata ya Nzihi katika Jimbo la Kalenga ili kuona katika eneo hilo ni eneo gani linafaa kuwa na kidato cha tano na sita, moja ya shule hizo tunaweza kupandisha hadhi ikawa kidato cha tano na sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nitumie nafasi hii kumsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, waanze kufanya tathmini hiyo kupitia wataalam wake na kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI, lakini pia kuanza kutenga mapato ya ndani kwa awamu kwa ajili ya kuanza kujenga baadhi ya miundombinu wakati Serikali pia ikitafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.(Makofi)
Name
Stella Ikupa Alex
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KASALALI E. MAGENI K.n.y. MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Shule za Sekondari Bulamba na Nansimo ili zitoe elimu ya kidato cha tano na sita?
Supplementary Question 4
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii.
Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba kuna utoshelevu wa walimu wa elimu maalum? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha miundombinu ya elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, pia walimu ambao wanafundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum na ndiyo maana vipo vyuo ambavyo vinafundisha walimu wenye uwezo wa kwenda kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum, lakini zipo shule ambazo zina miundombinu maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Stella Ikupa kwamba kama ambavyo Serikali imeendelea kuboresha miundombinu, walimu pamoja na vifaa vya kujifunzia na kufundishia wanafunzi wenye mahitaji maalum, itaendelea kufanya hivyo na kila kwenye bajeti ya kila mwaka wa fedha ikiwemo bajeti ya mwaka ujao 2025/2026, bajeti hiyo imetengwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunaboresha mazingira ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.