Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 41 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 521 2025-06-06

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. KASALALI E. MAGENI K.n.y. MHE. CHARLES M. KAJEGE aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Shule za Sekondari Bulamba na Nansimo ili zitoe elimu ya kidato cha tano na sita?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shule ya Sekondari Nansimo ilipata kibali cha kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa barua yenye Kumb. Na. EB.280/315/3816/10 ya tarehe 20/11/2023 ambapo jumla ya wanafunzi 176 wa kidato cha tano walipangiwa mwezi Julai, 2024. Aidha, shule tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Bunda zikijumuisha Chitengule ya Jimbo la Mwibara zipo kwenye mpango wa kupandishwa hadhi kuwa na kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2024/2025 Serikali imetoa shilingi milioni 130 kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja katika Shule ya Sekondari Chitengule kwa ajili ya maandalizi ya kuipandisha hadhi kuwa ya kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kukamilisha ujenzi wa miundombinu katika shule za sekondari zilizo kwenye mpango wa halmashauri kwa ajili ya kupandishwa hadhi kuwa za kidato cha tano na sita.