Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Kishapu?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali iliweka katika mpango wa bajeti kutekeleza ujenzi wa Magereza hii ya Wilaya ya Kishapu lakini kwa bahati mbaya mpaka hatua hii ya mwisho utekelezaji wake haujatekelezwa. Je, Serikali iko tayari kuwahakikishia wananchi wa Kishapu kwamba Magereza hii itaenda kujengwa katika mwaka wa fedha unaokuja (2025/2026)? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuna changamoto kubwa ya usafiri na hasa kwa wale mahabusu ambao wanakuwa na mashauri katika Mahakama iliyopo katika Wilaya ya Kishapu na inawabidi wasafirishwe kwenda Manispaa ya Shinyanga kuliko na Magereza ya Mkoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba inawapatia Mahakama ya Wilaya ya Kishapu na magereza kuhakikisha kwamba wanapata usafiri ambao utasaidia mahabusu hukudhuria mashauri kwa wakati bila usumbufu wa aina yoyote? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake katika ujenzi wa gereza katika eneo la Kishapu. Ni kweli, kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Gereza la Kishapu lilikuwa limewekwa kwenye mpango, lakini halikutengewa bajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na wananchi wa Kishapu kwamba kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ndiyo tunatenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa magereza hapo Kishapu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu gari, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshaagiza magari 11, kwa takribani shilingi bilioni 2.5. Basi Wizara ya Kishapu pia tutaiweka kwenye mpango ili wapate gari kwa ajili ya kusafirisha mahabusu kwenda kusikiliza mashauri yao katika Halmashauri ya Shinyanga, ahsante. (Makofi)
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Kishapu?
Supplementary Question 2
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna magereza ambayo yapo kwa ajili ya wafungwa kwa maana ya uzalishaji wa kilimo na mifugo takribani saba nchini yaliyojengwa enzi ya miaka ya 1970 ni ya matope, lakini sasa hivi yana wafungwa wachache, Askari Magereza wengi, hivyo hayana tija katika uzalishaji. Serikali haioni kwamba kuna umuhimu sasa wa kupunguza magereza haya yabaki walau mawili ili yaweze kuzalisha kwa tija? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Esther ametoa ushauri na sisi kama Serikali tunaupokea ushauri huo kwenda kuufanyia kazi tuone namna ya kuboresha eneo hilo, ahsante. (Makofi)
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Kishapu?
Supplementary Question 3
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana. Magereza nyingi nchini zina hali mbaya sana na ni chakavu. Ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha mnakarabati Magereza haya ili yawe katika hali nzuri au kujenga Magereza mpya nzuri na za kisasa ambazo zinaendana na wakati?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa Serikali ni kuzikarabati Magereza zote, ndiyo maana hata mwaka wa fedha huu wa 2025/2026 tumetenga shilingi bilioni 6.27 kwa ajili ya kufanyia ukarabati Gereza la Keko, Segerea, pamoja na Lilungu lililoko Mkoa wa Mtwara, ahsante.
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Primary Question
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Kishapu?
Supplementary Question 4
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi. Gereza la Mji wa Babati ni gereza linalotumika na Mkoa mzima wa Manyara; na wafungwa na mahabusu wamekuwa ni wengi, nafasi hazitoshi kabisa. Je, nini mkakati wa Serikali kujenga Gereza la Mji wa Babati ambalo ni la Mkoa? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Gereza la Babati ni dogo na kama alivyosema lina msongamano mkubwa, lakini tutaliweka kwenye mpango wa Gereza la Mkoa wa Manyara ili tuhakikishe tunajenga gereza kubwa linalotosheleza mahabusu pamoja na wafungwa katika eneo hilo, ahsante. (Makofi)
Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tanganyika
Primary Question
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Kishapu?
Supplementary Question 5
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Gereza la Kilimo la Kalilankulukulu ni gereza la muda mrefu, lina uchakavu wa hali ya juu na halina nyumba za watumishi. Je, ni lini Serikali itaenda kupeleka fedha za ukarabati wa gereza na kujenga nyumba za watumishi? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, Serikali ina mpango wa kukarabati hayo Magereza, lakini hatuwezi kukarabati kwa mwaka mmoja. Kwa hiyo, kila mwaka tunatenga bajeti kwa mwaka. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, pia gereza lake ambalo amelitaja, tutaliweka kwenye mpango ili kutengewa fedha kwa ajili ya ukarabati wa uhakika, ahsante. (Makofi)
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Kishapu?
Supplementary Question 6
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Lini Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kutembelea Gereza letu zuri la Kiberege kujionea miradi yetu mizuri na kuunga mkono miradi ya gereza? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakaa na Mheshimiwa Mbunge ili tupange namna ya kwenda kuona kazi kubwa inayofanyika katika gereza hilo, ahsante sana. (Makofi)