Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 37 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 479 | 2025-06-02 |
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Gereza la Wilaya ya Kishapu?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kishapu iliyopo Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa wilaya 50 nchini ambazo hazina Magereza. Aidha, mchakato wa maandalizi ya ujenzi wa Gereza la Wilaya Kishapu umekamilika sambamba na upatikanaji wa eneo la ekari 200 na zoezi la kuwalipa fidia wananchi wanaopisha eneo la ujenzi wa gereza limekamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ujenzi wa Gereza hilo utaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2027 kupitia mpango mahsusi wa ujenzi wa magereza mapya kwenye wilaya zisizokuwa na magereza nchini, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved