Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hassan Seleman Mtenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Primary Question
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Eneo la Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani? (Makofi)
Supplementary Question 1
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakushukuru kwa nafasi. Pia naishukuru Serikali kwa majibu mazuri na ninamshukuru Naibu Waziri kwa kweli kazi anayoifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli Serikali imejenga minara maeneo tajwa, lakini eneo la Naliendele ya Chini, tukizungumza maeneo ya Naulongo, na kuelekea mpaka kwenye hospitali ya kanda pale hakuna mawasiliano. Je, ni lini Serikali itakuja kutujengea minara hiyo ili hospitali ya kanda na maeneo mengine niliyoyazungumza tupate mawasiliano? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nipokee shukrani za Mheshimiwa Mbunge, na pia nikushukuru kwa kunipongeza mimi binafsi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo haya aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge, nikuhakikishie mwaka ujao wa fedha (2025/2026) tutahakikisha Maeneo ya Naliendele ya Chini yanaweza kujengewa minara, mawasiliano yawe ya uhakika. Vilevile, kwenye hospitali ya kanda, wito wetu ni kuhakikisha maeneo yote yanayotoa huduma za umma kama hospitali na shule yanapata mawasiliano ya uhakika. (Makofi)
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Eneo la Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani? (Makofi)
Supplementary Question 2
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza, nitoe pongezi kwa Serikali kutujengea mnara mzuri sana pale Mwakashindye. Nina swali la nyongeza. Lini Serikali itajenga mnara katika Kijiji cha Mbeya, Kata ya Igulungu?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Maige kwa ufuatiliaji, na juzi tu tulikuwa pamoja jimboni kwake kwenye ziara ya kuhakikisha mawasiliano yanapatikana maeneo yote. Kijiji cha Mbeya kipo kwenye utaratibu, mwaka ujao wa fedha (2025/2026) na chenyewe tutakifikia kuhakikisha mawasiliano yanakaa vizuri. (Makofi)
Name
Samweli Xaday Hhayuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hanang'
Primary Question
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Eneo la Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani? (Makofi)
Supplementary Question 3
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwezesha hii mitandao ya simu iwe inaingiliana, badala ya sasa hivi mtu kwa wilaya kubwa kama ya Hanang ili uwe na uhakika wa kupata mawasiliano kila sehemu lazima uwe na simu zaidi ya nne? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari mkakati unafanya kazi. Tumeshawaelekeza watoa huduma kama mwenzake ameshajenga mnara pale, basi waweze kutumia ule mnara kwa umoja wao. Vilevile tayari tunao mkakati wa kuona kwamba unatumia line moja kwa watoa huduma wote, pia michakato inaendelea. Lengo ni kuhakikisha mtu anatumia simu moja kumpunguzia mizigo. (Makofi)
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Eneo la Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani? (Makofi)
Supplementary Question 4
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri kwamba, ni lini mtarekebisha mawasiliano kutoka Njombe mpaka Songea? Maana yake pale katikati tukifika tu Njombe, ndiyo hatuwezi kuwasiliana kabisa na ndugu. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara kwa ufuatiliaji wa mawasiliano ya uhakika eneo la Njombe – Songea, naomba niwe nimepokea. Wataalam watakwenda kulifanyika tathmini na kuhakikisha linafanyiwa kazi. (Makofi)
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Eneo la Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani? (Makofi)
Supplementary Question 5
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nilitaka kujua kwamba ni lini Serikali itatujengea mnara kwenye Kijiji cha Masileye kwenye Kata ya Pagwi? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nimpongeze Mheshimiwa Omari Kigua; lengo la Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote tunavifikia na kupata mawasiliano ya uhakika. Kwa hiyo, Kijiji hiki alichokitaja Mheshimiwa Mbunge, Masileye na chenyewe tutahakikisha mwaka ujao wa fedha (2025/2026) kinakuja kufanyiwa tathmini na kuhakikisha mawasiliano ya uhakika yanawafikia. (Makofi)
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga mnara katika Eneo la Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani? (Makofi)
Supplementary Question 6
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Je, ni lini Serikali itahakikisha kwamba mtandao wa mawasiliano ya simu yanapatikana along the way SGR yote kuanzia Dodoma mpaka Dar es Salaam? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Kandege kwa ufuatiliaji wa mawasiliano ya uhakika. Katika barabara nzima ya SGR tayari wataalam wamefanya tathmini, na kazi inaendelea kuhakikisha barabara nzima toka tunavyotokea Dodoma mpaka Dar es Salaam watu waweze kupatikana bila kukatika mahali popote. (Makofi)