Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 37 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 478 2025-06-02

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga mnara katika Eneo la Mbawala Chini, Kata ya Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Naliendele ipo Minara ya Mawasiliano ya simu iliyojengwa na watoa huduma ambao ni Kampuni ya Airtel, Vodacom na Honora. Minara hii inatoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge ameuliza swali kuhusu kujengwa kwa mnara katika kata tajwa, inaashiria kuwa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa mawasiliano ya simu. Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itafanya tathmini kwenye kata tajwa ili kubaini mahitaji halisi ya mawasiliano ya simu, na endapo ikibainika kuwepo kwa tatizo la mawasiliano katika kata husika, itaingizwa katika zabuni ya miradi itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026. (Makofi)