Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rashid Abdallah Shangazi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlalo
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha Ilani za Uchaguzi za Vyama vya Siasa zinaendana na Dira ya Taifa?
Supplementary Question 1
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri kabisa ya Serikali, lakini nina jambo moja la nyongeza, aidha likawa swali ama ni ushauri. Kwa kuwa linazungumzwa kama ni hiari, lakini kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inalihusu Taifa letu, kwa nini Serikali isiweke mkazo na msisitizo kwamba vyama vyote vinavyotengeneza Ilani ni lazima ziakisi Dira ya Maendeleo ya Taifa?
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Dira ya Taifa Maendeleo rasimu yake italetwa hapa Bungeni kujadiliwa, na Bunge ndilo litakaloidhinisha, kwa hiyo, kama hayo ndiyo yatakuwa mapendekezo au matakwa ya Wabunge, ninadhani muda ukifika tutajadiliana na wakiweka hivyo tutaliweka. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved