Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 37 | Planning and Investment | Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji). | 475 | 2025-06-02 |
Name
Dr. Josephat Mathias Gwajima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kawe
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza: -
Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha Ilani za Uchaguzi za Vyama vya Siasa zinaendana na Dira ya Taifa?
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Askofu Josephat Mathias Gwajima, Mbunge wa Kawe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchakato wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo umeshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa. Kwa mfano, mnamo tarehe 21 Agosti, 2024 Msajili wa Vyama vya Siasa aliandaa kikao cha vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini, kwa lengo la kuwapa nafasi viongozi wa vyama hivyo kutoa maoni yao kuhusu Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kikao hiki pamoja na mambo mengine, viongozi wa vyama vya siasa walitoa maoni na kukubaliana kuwa maudhui ya Ilani ya vyama vyao kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 yaakisi maudhui ya Dira 2050. Hivyo, Serikali inaamini kuwa vyama vya siasa vitazingatia makubaliano yao na kutumia kikamilifu maudhui ya Rasimu ya Dira 2050 katika kuandaa Ilani ya vyama vyao vya siasa, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved