Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BAHATI K. NDINGO aliuliza: - Je, nini mkakati wa Serikali kusaidia upatikanaji wa majisafi na salama Mbarali kutoka 58% kufikia lengo la Serikali la 85%?
Supplementary Question 1
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa maswali mawili madogo ya nyongeza. Mbarali kuna vijiji 14 ambavyo havina maji kabisa: -
(a) Je, nini mkakati wa Serikali?
(b) Je, ni lini vijiji vya Matwebe, Maskuru, Lufingo, Masovo na Suma vitaondokana na shida ya maji?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Suma. Serikali inaendelea kuchukuwa hatua mbalimbali kuendelea kuhakikisha kwamba tunatatua changamoto ya maji. Vilevile nchi yetu yenye vijiji 12,318 na hatua iliyofanyika ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka hii minne ni hatua kubwa sana kutoka kwenye 75% mpaka sasa tumefikia 80% na kitu.
Mheshimiwa Spika, sasa tunatambua kwamba bado kuna vijiji ambavyo vitakuwa havijafikiwa; na huduma na ndiyo maana tunashukuru sana Bunge lako Tukufu kwa kupitisha bajeti ya kishindo ya Wizara ya Maji ya trilioni 1.016. Lengo lake ni kwenda kuhakikisha kwamba Watanzania wote wenye uhitaji wa maji wafikishiwe huduma ya majisafi na salama. Nina hakika vijiji 14 hivi vitakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwenda kuhakikisha kwamba wanapata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Spika, kwa swali la pili, ni kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi. Katika miradi hii ambayo itakwenda kukamilika na hayo maeneo ambayo ameyataja Mheshimiwa Mbunge na yenyewe yatakuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huo ambao utakuwa na suluhisho kwa wananchi katika maeneo haya.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved