Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 45 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 583 | 2025-06-12 |
Name
Bahati Keneth Ndingo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mbarali
Primary Question
MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. BAHATI K. NDINGO aliuliza: -
Je, nini mkakati wa Serikali kusaidia upatikanaji wa majisafi na salama Mbarali kutoka 58% kufikia lengo la Serikali la 85%?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama Wilayani Mbarali imepanda kutoka wastani wa 58% mwaka 2022 na kufikia 73% mwezi Desemba, 2024. Hali hii imechagizwa kutokana na kukamilika jumla ya miradi nane ya Mkunywa Awamu ya I & II, Igurusi Awamu ya I, Luduga – Mawindi Awamu ya 4&5, Magigiwe, Utengule usangu, Miyombweni, Mhwela – Mapogoro sanjari na mradi wa maji Matebetena ambapo kwa pamoja imewezesha vijiji 22 vya wilaya hiyo kufikiwa na huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Spika, vilevile, Serikali inaendelea na utekelezaji wa jumla ya miradi tisa kwenye Wilaya hiyo ambayo ni Ilongo – Group Awamu ya I, Isunura – Ikanutwa, Itamboleo Awamu ya II, Mbuyuni Awamu ya I, Warumba, Nyakazombe sanjari na upanuzi wa Skimu ya Maji Igava kwenda Vijiji vya Igunda, Muungano, Vikaye na Igava.
Mheshimiwa Spika, aidha, miradi mingine inayoendelea ni pamoja na ukarabati wa mradi wa maji Ruiwa Awamu ya I, ujenzi wa mradi wa maji Chimala pamoja na uchimbaji wa visima vitano na ujenzi wa miundombinu rahisi ya kutolea huduma kwa wananchi (point source).
Mheshimiwa Spika, miradi hiyo ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo inatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2025/2026 na kunufaisha zaidi ya watu 147,151 waishio kwenye vijiji 40 vya Wilaya ya Mbarali.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved