Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA K.n.y. MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: - Je, lini Visima vilivyochimbwa katika Kata za Mlingula, Mkwapa na Namatutwe – Masasi vitawekwa pampu?
Supplementary Question 1
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, pamoja na maswali mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini yeye mwenyewe aliahidi maji katika Kata ya Lipumburu, Kijiji cha Lipumburu wakati tulipokuwa tumefanya naye mkutano kwenye Kijiji cha Lupaso, je, anatekeleza lini ahadi hii ya uchimbaji wa kisima katika kata hii?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kati ya mikoa ambayo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi sana, ni katika huu Mkoa wa Mtwara ikiwemo mradi wa Makonde, mradi wa kutoka Ruvuma kwenda Mangaka Nanyumbu, mradi wa kuboresha miundombinu; na pia eneo lile ambalo Mheshimiwa Mbunge ametaja. Ni kweli kabisa nilifika mimi mwenyewe Lupaso na ni ahadi ya Serikali kwamba ni lazima kisima kichimbwe kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba fedha zipatikane ili tukatekeleze ahadi hiyo ya Serikali, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved