Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 45 Water and Irrigation Wizara ya Maji 582 2025-06-12

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA K.n.y. MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: -

Je, lini Visima vilivyochimbwa katika Kata za Mlingula, Mkwapa na Namatutwe – Masasi vitawekwa pampu?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Nia ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza inapatikana kwa wananchi wote nchini ikiwemo wananchi wa Kata za Mlingula na Namatutwe zilizopo Wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara. Katika kutimiza azma hiyo Serikali imekamilisha zoezi la ufungaji wa pampu kwenye visima vyote tisa vilivyochimbwa kwenye kata hizo na vimeanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.