Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa majengo ya utawala katika Shule za Sekondari za Choma, Ziba na Mwisi?
Supplementary Question 1
MHE. SEIF K. S. GULAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninamshukuru sana Serikali kwa fedha nyingi ambazo imezileta katika hizo shule, na kwa kutambua zile shule ambazo nimezitaja hapo, kwa maana ya Mwisi, Choma na Ziba kuwa ni shule za Kidato cha Tano na Sita; na kwa wingi wa wanafunzi ambao wanakwenda pale kwenye hizo shule walimu wanakosa sehemu ya jengo la utawala. Je, ni lini tatapata fedha kwa ajili ya shule hizo tatu za kimkakati za form five na form six?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Shule hizi za Sekondari Choma, Ziba na Mwisi ni shule za kidato cha tano na sita; na Serikali iliweka vipaumbele; kwanza, kuhakikisha kwamba miundombinu ya wanafunzi kusomea na kuishi katika shule hizo inakamilishwa ikiwemo mabweni, madarasa, vyoo na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa shughuli hizi zimeshatekelezwa, sasa kipaumbele cha pili ni kujenga majengo ya utawala. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Gulamali kwamba Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo ya utawala. (Makofi)
Name
Deo Kasenyenda Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makambako
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa majengo ya utawala katika Shule za Sekondari za Choma, Ziba na Mwisi?
Supplementary Question 2
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi. Kwa kuwa Serikali ilitupa fedha shilingi milioni 585 kwa ajili ya kujenga shule ya ufundi katika Jimbo la Makambako, je, ni lini Serikali itatupa fedha kwa ajili ya kukamilisha shule ya ufundi katika Mji wa Makambako?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali ilishapeleka fedha katika Halmahsauri ya Mji wa Makambako shilingi milioni 585 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari za amali ama ufundi. Tunafahamu kwamba ile ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa shule hizo, na shule hizo zimejengwa katika majimbo mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, awamu hiyo ya kwanza tayari shughuli za ujenzi zinaendelea. Serikali inaandaa mpango wa awamu ya pili kwa ajili ya kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu inayobaki. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa shughuli hiyo pia itatekelezwa.
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa majengo ya utawala katika Shule za Sekondari za Choma, Ziba na Mwisi?
Supplementary Question 3
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Serikali imekuwa ikipeleka fedha kwa ajili ya kujenga vyoo kwenye shule za msingi na sekondari vya kutumia maji, bila kuweka specifications wala kuweka gharama za maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi vyoo vinajengwa vinapaswa kutumia maji na shule hazina maji. Je, Serikali ina mkakati gani, kwamba inavyopeleka vyoo vya maji iwe inaweka pia miundombinu ya maji ikiwepo Shule ya Msingi Kitwechenkura na Omuchekano ambao wana vyoo wanabaki kuviangalia tu kwa sababu hawana maji?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeweka kipaumbele kwamba katika taasisi zote za umma lazima huduma za kijamii kama maji, umeme, barabara na kadhalika iwe ni kipaumbele namba moja. Kwa hiyo, katika shule hizo ninaomba nitumie nafasi hii kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kyerwa kuhakikishwa kwamba anawasiliana na RUWASA katika eneo husika ili waweze kupekeka maji mapema iwezekanavyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia maeneo yote kote nchini ujenzi wa vyoo vya maji unakwenda sambamba na ujenzi wa miundiombinu na maji.
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa majengo ya utawala katika Shule za Sekondari za Choma, Ziba na Mwisi?
Supplementary Question 4
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Shule nyingi zilizopo katika Jimbo la Kalenga zina changamoto ya majengo ya utawala, hususan Shule ya Sekondari ya Muhwana ambayo ipo katika Kata ya Magulilwa, walimu wanakaa kwenye madarasa hawana majengo ya utawala wala samani za kutumia walimu hawa. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili kujenga majengo ya utawala katika maeneo hayo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua kwamba zipo shule ambazo zina upungufu wa miundombinu yakiwemo majengo ya utawala, ikiwemo shule ya sekondari ambayo ipo katika Jimbo la Kalenga ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kupitia Mpango wa SEQUIP na programu mbalimbali za Serikali, tayari imeainisha shule zote zenye upungufu wa majengo ya utawala. Katika mwaka ujao wa fedha tutaendelea na ujenzi wa majengo ya utawala na tutahakikisha shule hiyo tunaipatia kipaumbele.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved