Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 37 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 474 | 2025-06-02 |
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: -
Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa majengo ya utawala katika Shule za Sekondari za Choma, Ziba na Mwisi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) aliuliza:
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa shule kuwa na miundombinu yote muhimu ikiwa ni pamoja na majengo ya utawala. Aidha, kwa sasa Serikali imejikita katika ujenzi wa madarasa, vyoo, mabweni na nyumba za walimu katika shule za sekondari ili kuendana na ongezeko la wanafunzi katika ngazi zote za sekondari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetoa shilingi milioni 777.71 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Choma, mabweni mawili, madarasa manne na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Ziba na ukamilishaji wa bwalo moja katika Shule ya Sekondari Mwisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za sekondari, ikiwa ni pamoja na majengo ya utawala. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved