Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Innocent Sebba Bilakwate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji Kata ya Songambele, Kyerwa?
Supplementary Question 1
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, naishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali ambazo wamekuwa wakichukua kuwapatia wananchi wa Wilaya ya Kyerwa maji safi na salama. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Mradi wa Lunyinya, Rwabwere mpaka Chanya umesimama kwa sababu ya mkandarasi anadai zaidi ya bilioni mbili. Ni lini mkandarasi atalipwa ili mradi huu uweze kukamilika? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Mradi wa Isingirio, Rutunguru na Kilela, awamu ya kwanza imekamilika. Ni lini awamu ya pili itaanza ili wananchi waweze kupata maji safi na salama? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Namshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Innocent Bilakwate kwa kuendelea kuwapigania wananchi wake na kwa kazi nzuri ya kushirikiana na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Ni dhamira ya Serikali kuhakikisha miradi yote inakamilika na wakandarasi wote wanalipwa hati zao za madai, ili miradi iendelee kutekelezwa na ikamilike kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mradi wa Lunyinya na Rwabwere pamoja na Chanya, ambao mpaka sasa mkandarasi alikuwa na hati ya madai ya bilioni 2.2 tayari tumeshawasilisha Hazina, kwa ajili ya malipo ya mkandarasi huyu.
Mheshimiwa Spika, vilevile Mradi wa Kilela, Isingiro pamoja na Rutunguru, ni kweli kabisa tumeshakamilisha awamu ya kwanza na sasa Serikali imeshauweka katika Bajeti ya Fedha ya 2025/2026, kwa ajili ya kuhakikisha tunaingia sasa kwenye awamu ya pili. Nimtoe hofu, Serikali inaendelea kutafuta fedha na zitakapopatikana tu, tayari tutaanza awamu ya pili katika mradi huu. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji Kata ya Songambele, Kyerwa?
Supplementary Question 2
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali sasa itakamilisha mradi wa Jeti-Buza na Kigamboni KK ili kuimarisha kupatikana kwa maji safi na salama katika Jimbo la Temeke?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana na ninamshukuru sana dada yangu kwa kuendelea kuwapigania Wanatemeke na kwa kazi nzuri ambayo anaendelea kuifanya. Ninakumbuka wiki iliyopita pia aliongelea kuhusu mradi huu.
Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, Serikali dhamira yake ni kuhakikisha kwamba Jimbo la Temeke ikiwemo Jeti pamoja na Buza, mradi huu ni kipaumbele chetu sisi kama Serikali kwa sababu upo katika utekelezaji wa Ilani. Tutahakikisha kwamba mradi huu unakamilika ndani ya mkataba ambavyo tulisaini na mkandarasi, ahsante.
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji Kata ya Songambele, Kyerwa?
Supplementary Question 3
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Spika, ninashukuru. Wananchi wa Kata ya Chitete iliyopo ndani ya Wilaya ya Ileje wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa maji. Ninataka kujua, je, ni lini Serikali watakamilisha mradi wa maji wa Mtembo Msia ili kurahisisha huduma kwa wananchi wetu wa Kata ya Chitete?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru, na ninamshukuru sana dada yangu Stella. Hakika Wanaileje wanahitaji huduma ya majisafi na salama, na mradi huu ninafahamu pia kuwa ni kipaumbele, hasa katika hii Kata ya Chitete. Mimi ninafahamu kabisa kwamba huu mradi upo katika progress nzuri.
Mheshimiwa Spika, na tuna mkataba, na ndani ya mkataba bado hatujaenda nje ya mkataba, kwa hiyo, tunaamini kabisa kwamba mradi huu utakamilika kulingana na mkataba ambao tulisaini na mkandarasi. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved