Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 45 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 581 | 2025-06-12 |
Name
Innocent Sebba Bilakwate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyerwa
Primary Question
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji Kata ya Songambele, Kyerwa?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inapatikana kwa wananchi wote waishio vijijini, wakiwemo wananchi wa Kata ya Songambele iliyopo Wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali kupitia mpango wa muda mfupi wa Programu Maalum ya Uchimbaji wa Visima 900, imekamilisha uchimbaji wa kisima kirefu pamoja na ujenzi wa miundombinu rahisi ya kutolea huduma kwa wananchi (point source) katika Kijiji na Kata ya Songambele na wananchi wanapata huduma. Aidha, katika mpango wa muda mrefu, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 itaanza kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa usambazaji maji katika Vijiji vya Kata ya Songambele.
Mheshimiwa Spika, miongoni mwa kazi zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 300,000, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 21 sanjari na ujenzi wa vituo 23 vya kuchotea maji. Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa ndani ya miezi nane, ambapo utanufaisha zaidi ya wananchi 18,404 waishio kwenye Vijiji vya Kata ya Songambele. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved