Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 1

MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ambayo yanaonesha kwamba kuna umuhimu mkubwa sana wa ujenzi wa hili daraja kutokana na kwamba wananchi wangu wengi walishakufa na bado wanatembea umbali mrefu kufuata shughuli zao; na kwa sababu daraja hili kuna mto katikati na barabara ya kutoka Mwanduti mpaka Ibambo hakuna; je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kuipandisha hadhi barabara hiyo ya kutoka Mwanduti mpaka Ibambo ili iweze kuhudumiwa na TARURA?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Wananchi wa Kijiji cha Ng’wande na Mwanduti wamefanya jitihada kubwa sana za kuchonga barabara wao wenyewe kwa nguvu zao, lakini barabara hiyo haina viwango na inahitaji umuhimu wa kuwekewa madaraja na makalavati. Je, Serikali inawaunga vipi mkono wananchi wangu hawa kwa kuwapelekea madaraja na makalavati, ili barabara hiyo iweze kupitika katika vipindi vyote vya mwaka?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Utaratibu wa kuziingiza barabara zetu kwenye mtandao wa TARURA, kwa maana ya kuzisajili, ni kwa halmashauri husika kuanza kwa kufanya maombi maalum Ofisi ya Rais, TAMISEMI kupitia kwa Katibu Tawala Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi tutafanya utaratibu wa kupandisha hadhi na kuzisajili barabara hizo katika mtandao wa TARURA. Kwa hiyo, ninaomba kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Migilla kwamba Serikali inathamini umuhimu wa miundombinu kuwa salama na bora kwa shughuli za kiuchumi na za kijamiii kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupitia halmashauri hiyo tuanze utaratibu wa kuomba kupandisha hadhi na kuisajili barabara hiyo ya kutoka Mwanduti kwenda Ibambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kaliua kuleta maombi hayo kwa kufuata utaratibu kwa kushirikiana na Meneja wa TARURA, ili Serikali ianze hatua ya kutathmini, kuona vigezo na pia kupandisha hadhi wakati tunajiandaa kujenga daraja hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, tunafahamu kwamba yapo maeneo ambayo wananchi wanajitolea nguvu zao. Nitumie nafasi hii kawapongeza wananchi wa kijiji hicho. Niwahakikishie kwamba, mara baada ya barabara hiyo kusajiliwa, Serikali itaiweka kwenye Bajeti ya TARURA, ili iweze kulimwa na kujengewa makalavati na madaraja, wananchi waweze kusafiri kwa usalama zaidi. (Makofi)

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 2

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Je, ni lini Serikali itatenga fedha ili kujenga daraja linalounganisha kati ya Kitongoji cha Nyakasoma, Kijiji cha Isima Jimboni Busanda kwenda Kijiji cha Chibumba Jimboni Chato? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba daraja la eneo la Nyakasoma kwenda Chibunda ni daraja muhimu, ni kubwa na Serikali inatambua umuhimu wa kujenga daraja hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tayari Serikali imeanza kufanya usanifu wa ujenzi wa daraja hilo; na tumeshamwelekeza Meneja wa TARURA Mkoa wa Geita na Wilaya ya Geita kuleta taarifa ya usanifu wa kina na kuleta makadirio ya ujenzi wa daraja hilo ili Serikali iweze kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi huo. (Makofi)

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Halmashauri ya Manyoni kuna Madaraja ya Kapiti na Magasai ambayo yamekuwa kikwazo kikubwa sana cha wananchi kusafiri. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba wananusuru wananchi hawa kwa kujenga madaraja hayo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya tathmini na kuainisha maeneo yote korofi katika halmashauri na majimbo yote likiwemo Jimbo la Manyoni katika Daraja hilo la Kapiti na Makasai. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa madaraja hayo kwa awamu ili kuhakikisha kwamba wananchi wanasafiri na kupita kwa usalama zaidi. (Makofi)

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 4

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itatenga fedha za kutosha ili kujenga daraja linalounganisha Kata ya Malatani na Kata ya Nanyumbu kwenye Kijiji cha Chitoha ambalo limekuwa kero sana kwa wananchi hao?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI nimwelekeze Meneja wa TARURA wa Halmashauri ya Nanyumbu pamoja na Meneja wa TARURA Mkoa wa Mtwara kutuletea taarifa rasmi ya usanifu na mahitaji ya fedha katika ujenzi wa daraja hilo muhimu, ili Serikali ione namna ya kutafuta fedha kwa awamu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja hilo.

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 5

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Katika Kata ya Mbokomu daraja limefunikwa na kifusi baada ya maafa kutokea Mbokomu kwenda Kidia, pia barabara hii haipitiki kabisa tangu maafa haya yametokea, je, Serikali ina mkakati gani wa kurekebisha mundombinu hii ili kuruhusu wananchi waweze kufanya shughuli zao za maendeleo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli hapa katikati tulipata baraka ya mvua nyingi, lakini ilikuja na changamoto kwa kuharibu miundombinu, likiwemo daraja hili la Mbokomu – Kidia katika Mkoa wa kilimanjario Jimbo la Vunjo (Moshi Vijijini). Ninaomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwanza Serikali imeshatoa maelekezo kwa mameneja wote wa TARURA kote nchini kufanya tathmini ya barabara zilizoharibiwa na mafuriko na kutuwasilishia Ofisi ya Rais, TAMISEMI (TARURA) kwa ajili ya kufanya matengenezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari Serikali imeanza kutoa fedha kwa awamu katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madaraja hayo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali italifikia daraja hilo, tutafanyia matengenezo pamoja na barabara ili kuhakikisha kuwa tunalirejesha kwenye hali nzuri.

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 6

MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, madaraja ya Ujaile pamoja na Kimbwi yalizolewa na mvua wakati wa mvua kubwa, je, Serikali ina mpango gani wa kuyajenga madaraja haya, likiwemo Daraja la Ujaile ambalo tayari IMF walishatoa fedha ili kumpata mkandarasi kumaliza tatizo hilo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, Serikali imekwishatoa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja hilo la Ujaile. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba taratibu za kuanza ujenzi zipo mwishoni, na tunatarajia wakati wowote kazi ya ujenzi itaanza. (Makofi)

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 7

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Barabara inayotoka Liwale kwenda kwenye Kata ya Mpigamiti ina daraja la Ngorongopa ambalo ni chakavu sana. Je, ni lini Serikali itatupatia fedha kujenga Daraja hilo la Ngorongopa pamoja na ukarabati wa barabara hiyo? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua umuhimu wa daraja lile la Ngorokomu na kwamba Mheshimiwa Mbunge amefuatilia mara kadhaa na nimhakikishie kwamba sisi kama Serikali tayari tumeliwekea mpango madhubuti kabisa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati maeneo mbalimbali ya barabara hiyo.

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 8

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Moshi Mjini ipo katika Mradi wa TACTIC Tyre Two. Barabara inayoanzia Kata ya Ng’ambo – Miembeni – Msaranga – Njoro inalo Daraja la Otieno ambalo tunategemea litengenezwe na mradi huu. Je, ni nini kinachokwamisha kusainiwa kwa mkandarasi kwa ajili ya barabara hizi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatekeleza mpango wa kukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali kupitia Mpango wa TACTIC, na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ni moja ya halmashauri zilizokuwa awamu ya pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba hakuna kinachokwamisha kusaini mkataba. Tupo kwenye hatua za kawaida za manunuzi na wakati wowote mkataba utasainiwa na barabara hiyo pamoja na daraja hilo vitajengwa kupitia Mpango wa TACTIC.

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: - Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Supplementary Question 9

MHE. USSI S. PONDEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nilikuwa ninataka nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba Daraja la Ibukilo kwenda Kata ya Sengo ambalo lipo Wilayani Maswa limeahidiwa na TARURA litajengwa. Je, ni lini ujenzi wake utaanza?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua umuhimu wa daraja hilo na imeendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya kujenga madaraja yote ya kimkakati katika maeneo ambayo yameharibiwa na mvua, na daraja hilo katika Halmashauri ya Maswa litajengwa.