Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 37 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 473 2025-06-02

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: -

Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa Daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo katika Kata ya Mwongozo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha usanifu wa awali wa daraja linalounganisha Kijiji cha Mwanduti na Ibambo. Aidha, usanifu wa kina umepangwa kufanyika katika mwaka wa fedha 2025/2026 kwa lengo la kubaini gharama halisi za ujenzi, mahitaji ya kiufundi na maandalizi ya nyaraka za zabuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya usanifu wa kina kukamilika, Serikali itatafuta fedha za ujenzi wa daraja hilo ili kutatua changamoto ya mawasiliano katika Vijiji vya Mwanduti na Ibambo.