Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, kwanza, naishukuru Serikali kwamba, imeanza kuonesha nia ya kuijenga barabara hii ambayo kwa kweli, ina matumizi makubwa sana ya wananchi. Nachukua nafasi hii pia, kuiomba Serikali, kwanza kuwauliza ni lini utaratibu huu utakamilika, ili mkataba uweze kusainiwa na barabara ianze kujengwa kwa sababu, wananchi wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu sana na, Mbunge, Mheshimiwa Juliana Shonza amekuwa akiipigania sana barabara hii?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili kwa ajili ya Jimbo la Makete. Tuna barabara ya kutoka Chimala kuelekea Matamba kuja Kitulo, kilometa 51; ni lini upembuzi yakinifu utakamilika ili barabara hii ianze kujengwa kwa kiwango cha lami kwa sababu, kwenye bajeti imeoneshwa kwamba, mna nia ya kuijenga barabara hii? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, napenda kumjulisha tu Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wa Majimbo hayo, Mheshimiwa Shonza, Mheshimiwa George Mwenisongole na Mheshimiwa Condester Sichalwe, ambao barabara hizo zinawahusu kwamba, mkataba umekamilika. Sasa tunachofanya tu ni siku ya kusaini huo mkataba kwa sababu, mkandarasi ameshapatikana na documents zote ziko tayari, kwa ajili ya kusaini kuanza huo ujenzi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili, kwanza n Mheshimiwa Mbunge, atakubaliana nami kwamba, hii barabara ilikuwa chini ya TARURA, imeshapanda hadhi na sasa hivi tunaiingiza kuanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ili iweze kuendana na standard za TANROADS na pia, ikiwa ni maandilizi ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Supplementary Question 2

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, barabara inayotoka Handeni kupitia Kata ya Negero hadi Mziha, kwa kipindi hiki kuna mashimo mengi sana baada ya mvua kunyesha. Je, nini mpango wa Serikali, ili kufukia mashimo hayo kabla ya kufanya ukarabati mkubwa? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naomba tu nitumie nafasi hii kumwelekeza Meneja wa Mkoa wa Tanga kwamba, baada ya kipindi cha mvua kwisha, aweze kuhakikisha kwamba, hii barabara inakwenda kukarabatiwa kwa sababu bajeti imeshatengwa, lakini kwa kuwa, mvua imekatika, basi ni muda sahihi sana wa kwenda kuikarabati, ikiwa ni pamoja na kuziba hayo mashimo, ili wananchi waweze kufanya shughuli zao za usafiri na usafirishaji kwa uhakika. Ahsante. (Makofi)

Name

Catherine Valentine Magige

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Supplementary Question 3

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Barabara inayotokea Babati kuelekea Makuyuni imeharibika sana na imekuwa inaleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji. Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha barabara hii inakarabatiwa haraka sana? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, hata katika bajeti yetu tuliyoipitisha, fedha nyingi sana tumezielekeza kwenye ukarabati wa barabara na barabara aliyoitaja, hii ni barabara kuu ambayo inaanzia Dodoma – Kondoa – Babati – Makuyuni kwenda Arusha. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Wizara tayari imeshaainisha barabara hizo, ikiwa ni pamoja na kipande hiki cha Babati – Makuyuni kuhakikisha kwamba, zinafanyiwa ukarabati. Ahsante. (Makofi)

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itajenga barabara inayotoka Makao Makuu ya Kilolo kwenda Kising’a – Ukwega – Wotalisoli – Mlafu mpaka Ilula, ili wananchi wasipate adha ya kuzunguka mpaka mjini kwenda Makao Makuu yao ya Kilolo? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, barabara hii kimsingi bado haijafanyiwa upembuzi yakinifu. Tumeshapata maombi, kwa maana ya mapendekezo ya Mkoa wa Iringa kupitia kwa Meneja wa TANROAD kwamba, barabara hii tuweze kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandilizi kwa baadaye kuijenga kwa kiwango cha lami, lakini kwa sasa ni kuifanyia usanifu kuikarabati, ili ipitike mwaka mzima. Ahsante. (Makofi)

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Supplementary Question 5

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, Barabara ya Mlowo – Kamsamba, mkataba upo tayari. Sasa ni lini mkataba huo utaisaniwa kati ya Serikali na mkandarasi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa, kama nilivyosema, upo tayari. Tukubaliane na Mheshimiwa Mbunge, tungetamani pia, yeye mwenyewe ashuhudie wakati tunasaini. Tukubaliane lini tuusaini huo mkataba, lakini upo tayari. Ahsante.

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Supplementary Question 6

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, Barabara ya kutoka Buhigwe – Msalala – Kahama kwenda Mwakitolyo, Shinyanga ni barabara muhimu sana. Je, ni lini itajengwa kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara hii tumekuwa tukiijenga kwa awamu na hasa tumeanza kwenye vipande vya mji, lakini tumeshakamilisha usanifu. Tunachofanya sasa hivi ni kutafuta fedha ili kuijenga yote kwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Supplementary Question 7

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Barabara ya Makambako – Songea muda mrefu tumeambiwa kwamba, Serikali inaendelea kutafuta fedha na imefanya majadiliano. Je, imefikia wapi kupata hizo fedha? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, barabara ya Makambako – Songea, kwanza kipande cha kutoka Songea mpaka Lutukira, kama kilometa 92, tulishapata fedha kupitia World Bank mpango ambao una TANTIP na tayari tuko kwenye maandilizi ya kuanza kuijenga kwa sababu na mkandarasi ameshapatikana.

Mheshimiwa Spika, kutoka Lutukira – Njombe kuja Makambako, Serikali inaendelea kutafuta chanzo kikubwa cha uhakika cha fedha kwa sababu, ni moja ya barabara kubwa ambayo inatakiwa ikarabatiwe. Kweli tunakiri ni barabara ya zamani na ni kati ya barabara ambazo zimechoka sana, Serikali inaendelea kutafuta fedha, ili tuweze kuikarabati yote kama tutakavyofanya Songea hadi Lutukira. Ahsante. (Makofi)