Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 45 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 580 2025-06-12

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, lini ujenzi wa Barabara ya Mlowo – Kamsamba utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, taratibu za manunuzi ya mkandarasi, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kiwango cha lami wa kilometa tano kuanzia Mlowo kuelekea Kamsamba na nyingine tano kuanzia Kamsamba kuelekea Mlowo zipo katika hatua za mwisho (Negotiations). Taratibu za manunuzi zikikamilika na Mkandarasi wa ujenzi kupatikana, kazi ya ujenzi wa barabara hiyo utaanza. Ahsante.