Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Wodi za Wanaume na Wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Same?
Supplementary Question 1
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, kwanza naipongeza kwa hatua ambayo imefikia katika ujenzi wa hospitali hiyo, lakini nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hospitali hiyo, wodi ya akinamama na watoto imeanza kufanya kazi, lakini kuna changamoto ya wauguzi kutokuwa na nyumba za kuishi katika maeneo hayo. Je, ni mpango gani wa Serikali, wa haraka, wa kujenga nyumba za watumishi? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri kwa namna ambavyo amekuwa akiwasemea kwa dhati wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, namhakikishia tu kwamba, hoja yake mwanzo ilikuwa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri katika Wilaya ya Same. Tayari Serikali sikivu inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeshajenga. Imepeleka zaidi ya shilingi 3,400,000,000.00 na mwaka wa fedha ujao 2025/2026 tumetenga shilingi milioni 800, kwa ajili ya kujenga wodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ujenzi wa hivi vituo vya huduma na kupeleka vifaatiba na watumishi, Serikali imeweka mpango kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi. Kwa hiyo, nakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Hospitali ya Halmashauri ya Same ni moja ya hospitali ambazo zimetengewa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba za utumishi katika mwaka wa fedha ujao 2025/2026.
Name
Bupe Nelson Mwakang'ata
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Wodi za Wanaume na Wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Same?
Supplementary Question 2
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kituo cha Afya cha Kata ta Kilando hakina jengo la mortuary. Ni lini Serikali itajenga jengo hilo kwa Kata ya Kilando? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa Serikali ni kujenga majengo yote muhimu katika vituo vya afya, yakiwepo majengo ya kuhifadhia maiti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi hii nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika Kituo cha Afya cha Kilando, Serikali inatambua kuna baadhi ya majengo ambayo yanahitajika, likiwemo jengo hilo la kuhifadhia maiti, na tayari tumeweka mpango mkakati wa ukamilishaji wa majengo katika zahanati na vituo vyote ambavyo vina majengo pungufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaweka kipaumbele katika Kituo cha Afya cha Kilando, ili tuweze kujenga jengo hilo. (Makofi)
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Wodi za Wanaume na Wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Same?
Supplementary Question 3
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwanza naipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kukamilisha kutujengea Hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale. Pale kuna thamani nyingi, majengo yapo na wagonjwa wapo wengi. Je, Serikali ina mpango gani wa kutujengea uzio kwa ajili ya kulinda mali zilizopo pamoja na wagonjwa? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kujenga hospitali za Halmashauri, ikiwepo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, kama alivyosema Mheshimiwa Amar, lakini nakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge tumepanga na tumeweka vipaumbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele cha kwanza kilikuwa ni kuhakikisha majengo ya huduma yanakamilika, kupeleka vifaatiba na watumishi. Kwa kuwa tumekamilisha hilo, tutakwenda kipaumbele cha pili, kuangalia namna ya kuboresha usalama katika maeneo hayo, ikiwemo kujenga fence, uzio, katika hospitali hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi hii, kukuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwa kushirikiana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale pamoja na Serikali Kuu tutaendelea kutenga fedha kwa awamu, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uzio katika hospitali hiyo. (Makofi)
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Wodi za Wanaume na Wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Same?
Supplementary Question 4
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naishukuru sana Serikali kwa jinsi ambavyo mmeweza kutujengea Kituo cha Afya, Kata ya Kilakala na vifaa vyote vimeingia. Je, sasa Serikali ni lini itaanza kile Kituo cha Afya cha Kata ya Sandali, ndani ya Jimbo la Temeke?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Ndiyo maana hivi leo ninapoongea, Mheshimiwa Rais, ndani ya mwezi huu mmoja, ametoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya majimbo 120 katika maeneo ambayo Waheshimiwa Wabunge waliainisha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya. Kwa hiyo, hii ni dhamira ya dhati ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunatambua katika Jimbo la Temeke yapo maeneo ambayo, Serikali tayari imejenga vituo vya afya, lakini bado kuna kata za kimkakati. Nakuhakikishia tu kwamba, tutaendelea kutenga fedha kuhakikisha pia, katika kata hiyo tunapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya. Ahsante.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Wodi za Wanaume na Wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Same?
Supplementary Question 5
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Meatu ina hospitali ambayo ni kubwa, ina wodi moja ya wanaume na moja ya wanawake, lakini zile wodi hazitoshi, wagonjwa wanalala wawili wawili. Je, ni lini Serikali itaongeza wodi nyingine katika Hospitali hiyo ya Wilaya ya Meatu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ni moja ya hospitali kongwe. Tayari Serikali imepeleka fedha, kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa hospitali hiyo. Kazi imefanyika kwa ufanisi mkubwa na wananchi wanaendelea kupata huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, Serikali inatambua kwamba, pamoja na fedha zilizopelekwa bado kuna baadhi ya miundombinu inayopungua. Ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Minza kwamba, tunaendelea kupeleka fedha kwa awamu, kwa ajili ya kukamilisha miundombinu mingine ambayo imebaki. (Makofi)