Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 37 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 471 2025-06-02

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Wodi za Wanaume na Wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Same?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilianza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Same, Novemba, 2022. Hadi mwezi Aprili, 2025 Serikali imepeleka jumla ya shilingi bilioni 3.4, ambapo shilingi bilioni 2.6 zimetumika katika ujenzi wa majengo ya hospitali ya halmashauri hiyo na shilingi milioni 800 kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba. Aidha, majengo matano kati ya nane, ujenzi umekamilika na yameanza kutoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 imetenga shilingi milioni 800, kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanaume, wanawake, watoto na ujenzi wa njia za kutembea wagonjwa (Walkways) katika Hospitali ya Wilaya ya Same, ahsante.