Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: - Je, lini Serikali itaielekeza Halmashauri ya Msalala kuanza kulipa posho za Wenyeviti wa Vijiji?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu ya Naibu Waziri. Sasa kwa kuwa, fedha zilizotengwa ni nyingi ukilinganisha na ambazo zimetolewa, nini kauli ya Serikali?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nampongeza Mheshimiwa Christina Mnzava kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia ustawi wa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa. Nimhakikishie tu kwamba, kwanza Serikali hii inajali sana na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Waheshimiwa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa, ndiyo maana katika halmashauri zote 184 Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipa posho za kila mwezi za Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Msalala ilitenga shilingi milioni 11.04 na imelipa shilingi milioni 10.1 kwa maana ya kwamba, ifikapo tarehe 30 mwezi huu wa Juni, fedha hii yote itakuwa imeshalipwa na wale Waheshimiwa Wenyeviti watakuwa wamepata fedha zao zote. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itaendelea kulipa posho hizo kwa Wenyeviti wa Vijiji.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: - Je, lini Serikali itaielekeza Halmashauri ya Msalala kuanza kulipa posho za Wenyeviti wa Vijiji?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Madiwani wanafanya kazi kubwa sana kwenye Kata na Majimbo yetu, Serikali, inaonaje sasa iweke bayana ni kiasi gani cha posho ambayo inaenda kuongezwa? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli kwamba, Waheshimiwa Madiwani na Wahehsimiwa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa wanafanya kazi kubwa sana za uongozi katika maeneo yao. Serikali hii inatambua kazi nzuri inayofanywa na viongozi hao, ndiyo maana, kwanza kwa upande wa Waheshimiwa Madiwani, ilichukua jukumu la kulipa posho kwa Waheshimiwa Madiwani katika halmashauri zetu zote na inalipa kila mwezi kiwango ambacho kimewekwa kwa mujibu wa taratibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Waheshimiwa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa, halmashauri husika hutenga fedha kila mwaka kulingana na uwezo wa halmashauri husika. Kwa hiyo, natumia nafasi hii kwanza kumhakikishia, Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kulipa posho za Waheshimiwa Madiwani na Waheshimiwa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, tutaendelea kuona uwezekano, kwa kadiri ya uwezo wa Serikali, namna ambavyo halmashauri zitaboresha posho za Wenyeviti wa Vijiji. (Makofi)