Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 37 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 470 2025-06-02

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza: -

Je, lini Serikali itaielekeza Halmashauri ya Msalala kuanza kulipa posho za Wenyeviti wa Vijiji?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ina jumla ya vijiji 92 ambavyo vyote vina Wenyeviti wa Vijiji. Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Halmashauri ya Msalala ilitenga shilingi milioni 5.5, kwa ajili ya posho za Wenyeviti wa Vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025, halmashauri ilitenga shilingi milioni 11.04. Hadi Mei, 2025, shilingi milioni 10.1 zimelipwa na kiasi cha shilingi 920,000 kitalipwa kufikia Juni, 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga shilingi milioni 11.04, kwa ajili ya kuendelea kulipa posho za Wenyeviti wa Vijiji katika Halmashauri ya Msalala, ahsante.