Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati mkubwa Soko la Mbagala Kizuiani?

Supplementary Question 1

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Chamazi ni eneo lenye wakazi wengi, je, kwenye masoko yanayotegemewa kujengwa, itakuwemo na yenyewe kujengewa soko kubwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Soko la Karata na Mbande nalo limo kwenye mpango huo kufanyiwa ukarabati? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, tunafahamu kwamba Soko la Chamazi, Mbande na ambalo Mheshimiwa Mbunge amelitaja ni miongoni mwa masoko katika Manispaa ya Temeke ambayo nayo yanahitaji ukarabati na mengine ujenzi na kuongeza miundombinu muhimu.

Mheshimiwa Spika, katika mpango wa bajeti ya Manispaa ya Temeke kwa mwaka 2025/2026 masoko yaliyotengewa shilingi milioni 800 ni masoko matano ambayo ni Soko la Temeke Sterio, Tandika Kuu, Mbagala Kizuiani, Lumu, na Toangoma.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa awamu hiyo tutakwenda kukarabati masoko hayo Matano, lakini Serikali inatambua umuhimu wa kukarabati masoko hayo mengine pia, hivyo itaendelea kutenga bajeti kwa awamu ili tuyafikie na kuyakarabati.

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati mkubwa Soko la Mbagala Kizuiani?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Je, Wizara ya TAMISEMI inashirikianaje na Wizara ya Kilimo ili kuharakisha uboreshaji wa miundombinu kwenye masoko ya Kisambo, Himo, Mwika, na Marangu Mtoni? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inashirikiana kwa karibu sana na Wizara ya Kilimo katika masoko, hususan masoko yaliyoko mipakani katika Jimbo la Vunjo, Mwika, na mengine. Pia, yako masoko ambayo tayari hatua za ujenzi zinaendelea, lakini yako masoko ambayo tunaendelea kufanya tathmini na yatajengwa kwa Mfumo wa PPP.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Kimei hoja zake amezileta mara kadhaa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Kilimo tayari tumeanza utekelezaji na tunaamini wakati wowote tutaanza utekelezaji wa ujenzi wa masoko hayo.

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati mkubwa Soko la Mbagala Kizuiani?

Supplementary Question 3

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kuweka paa pamoja na sakafu kwenye Soko la Manyema, Moshi Mjini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninaomba nichukue hoja ya Mheshimiwa Priscus Tarimo, Mbunge wa Moshi Mjini, kuhusiana na uhitaji wa sakafu na paa katika soko hilo.

Mheshimiwa Spika, pia, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI nimwelekeze Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kuanza kufanya tathmini haraka iwezekanavyo kujua gharama ya matengenezo ya soko hilo na kuona uwezekano wa kuanza kutenga fedha kwa ajili ya mapato ya ndani kufanya kazi hiyo, na pia, kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI eneo la gap ambalo litapatikana ili Serikali pia iweze kuona namna ya kupeleka fedha.

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati mkubwa Soko la Mbagala Kizuiani?

Supplementary Question 4

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha biashara ya mpakani, ni lini sasa Serikali itajenga na kukamilisha soko kwenye mpaka kati ya Uganda na Tanzania pale Mutukula?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali ilishafanya tathmini ya masoko yote ya mpakani likiwemo soko lile la Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Mheshimiwa Spika, tayari tumeanza kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa ujenzi, upanuzi, na ukarabati wa masoko hayo. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mushashu kwamba, Soko la Mutukula ni moja ya masoko ambayo yameshaainishwa na ninakumbuka mwaka juzi 2023 tulipita pale kwenye ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na alitoa maelekezo hayo na Ofisi ya Rais, TAMISEMI tumeanza taratibu za utekelezaji.