Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 45 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 577 | 2025-06-12 |
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati mkubwa Soko la Mbagala Kizuiani?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetenga shilingi milioni 800 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa wa masoko yake likiwemo soko la Mbagala Kizuiani.
Mheshimiwa Spika, usanifu na upembuzi yakinifu wa mahitaji ya ukarabati wa soko la Mbagala Kizuiani umeshakamilika na utekelezaji wake utaanza mapema katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved