Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Simon Songe Lusengekile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busega

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 1

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali. Ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kwa kuwa sasa watu wa TARURA kule Nkasi wameshaleta maombi ya shilingi milioni 680 kwa ajili ya kuweka taa za barabarani, je, Serikali iko tayari sasa Julai kupeleka sehemu ya fedha ili waanze kuweka hizi taa za barabarani kama ilivyoombwa na TARURA?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Tuliahidiwa ujenzi wa stendi pale Lamadi. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi huu ili wananchi waweze kutumia stendi ambayo imeahidiwa na Serikali? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ni kweli kwamba, Mji wa Namanyere wameleta maombi ya kuweka taa barabarani na tayari Meneja wa TARURA Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa wamefanya tathmini na shilingi milioni 630 zinahitajika.

Mheshimiwa Spika, hatua ambayo inaendelea hivi sasa ni Serikali kufanya process za kupata fedha hizo kwa ajili ya kwenda kuanza kufunga taa katika Mji wa Namanyere kwa awamu. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Songe kwa niaba ya Mheshimiwa Aida Khenani kwamba, Serikali tayari imeshaanza mkakati wa kutafuta fedha kwa ajili ya kufunga taa hizo za barabarani na zoezi hilo litafanyika kwa awamu.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na uhitaji wa stendi katika Mji wa Lamadi, ni kweli na tayari maombi hayo ya Halmashauri ya Busega yamewasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI na tumeshaingiza kwenye mpango wa maeneo yanayohitaji kujengwa stendi za kimkakati. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Songe kwamba, Serikali itakwenda kutekeleza ahadi hiyo.

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 2

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Changamoto iliyopo Namanyere ni sawasawa na changamoto iliyopo katika Jimbo la Buhigwe Makao Makuu ya Wilaya ya Buhigwe. Lini Serikali itatujengea stendi ya kisasa katika Mji wetu wa Buhigwe? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali ilishaweka mpango mkakati wa utekelezaji kwa awamu kwa ajili ya kuhakikisha maeneo yote ambayo yanahitaji huduma za stendi kwa ajili ya kuboresha mapato ya ndani ya halmashauri na huduma za kijamii katika eneo la usafiri katika kila halmashauri zetu, yanaainishwa na yanaanza kutengewa fedha kupitia vyanzo vya ndani vya halmashauri kwa kadri ya uwezo wa halmashauri. Pia, lile pengo la bajeti liwasilishwe Ofisi ya Rais, TAMISEMI ili kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi hizo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nichukue nafasi hii nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buhigwe, kuanza kufanya tathmini ya mahitaji ya fedha katika eneo hilo la ujenzi wa stendi ili kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa ajili ya hatua zaidi za utekelezaji.

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 3

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI italeta fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ili kukamilisha ujenzi wa stendi pale Nangurukuru, ambayo halmashauri kupitia mapato yake ya ndani imeuanza?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa na Menejimenti nzima, Baraza la Madiwani na Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo yote mawili kwa kuanza kutoa fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi ya mabasi pale Nangurukuru.

Mheshimiwa Spika, hayo ndiyo maelekezo ya Serikali, kwamba halmashauri zianze kutenga fedha za mapato ya ndani badala ya kusubiri fedha zote kutoka Serikali Kuu na pale ambapo kunakuwa na pengo la ukamilishaji wawasilishe maombi hayo Ofisi ya Rais, TAMISEMI ili Serikali Kuu iweze kuona namna ya kuwaunga mkono na kukamilisha ujenzi huo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kassinge kwamba, hoja hiyo tumeichukua na tutaifanyia kazi kuona namna ambavyo tutatenga bajeti kwa ajili ya kwenda kumalizia ujenzi wa stendi pale Nangurukuru.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 4

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Kyela ni lini mtakuja kutuwekea taa katika stendi kuu pale?

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninaomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutawasiliana na uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela. Pia, nitumie nafasi hii kumwelekeza Meneja wa TARURA Mkoa wa Mbeya pamoja na Meneja wa TARURA Wilaya ya Kyela, wafanye tathmini ya mahitaji ya taa za pale stendi ili tuweze kuona namna ya kuanza kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji.

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 5

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Je, ni lini Serikali itatujengea stendi ya kisasa Ngara Mjini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Ngara imeshawasilisha pia maombi ya kujengewa stendi ya kisasa. Hata hivyo, tunafahamu kwamba, pamoja na kipaumbele cha stendi, kulikuwa na kipaumbele cha barabara, na tayari tumeanza utekelezaji wa barabara za pale Ngara Mjini.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Oliver Semuguruka kwamba, ombi hilo limefika Serikalini na Serikali inaendelea kufanya utaratibu kwa ajili ya kuanza kutenga fedha kwa mapato ya ndani ya halmashauri, lakini pia kutoka Serikali Kuu kwa awamu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi katika eneo la Ngara.

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 6

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Mji wa Kibara unakua kwa kasi sana. Je, ni lini Serikali itajenga stendi ya kisasa ili kusaidia wananchi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bunda na Baraza la Madiwani kuanza kufanya tathmini ya kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa stendi katika Mji wa Mwibara. Pia, waone gharama zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi na kuanza kutenga fedha za mapato ya ndani kwa awamu; na baadaye kuwasilisha maombi kwa ajili ya Serikali Kuu kuchangia nguvu hizo na kujenga stendi katika eneo la Mwibara.

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 7

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, Stendi ya Wilaya ya Mbozi pale Vwawa Mjini ni chakavu sana. Ni upi mkakati wa Wizara kuhakikisha inaboresha stendi ile? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ninafahamu kwamba stendi ile ni ya siku nyingi na ni chakavu, lakini Mheshimiwa Neema Mwandabila na Mbunge wa Jimbo hilo mara kadhaa wameulizia kuhusiana na ujenzi wa stendi hiyo na tayari tulishawasiliana na Mkurugenzi wa Mbozi na wameshawasilisha maombi ya fedha.

Mheshimiwa Spika, kinachofuata sasa ni kuona namna ambavyo tutaanza kutenga bajeti kwa awamu kupitia mapato ya ndani, lakini pia kupitia Serikali Kuu kwa ajili ya kuanza ujenzi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Neema Mwandabila na wananchi wa Vwawa pale Mbozi kwamba, Serikali imechukua hoja hiyo na inaendelea kuifanyia kazi.

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Supplementary Question 8

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itatujengea stendi ya kisasa katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Mkunwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, tunafahamu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini eneo la Mkunwa, kuna uhitaji wa ujenzi wa stendi na Mheshimiwa Shamsia amewasilisha mara kadhaa.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Mtwara Vijijini kwamba, Serikali hii sikivu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepokea hoja hiyo na itakwenda kuifanyia kazi.