Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 45 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 576 2025-06-12

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Stendi ya Kisasa na kuweka Taa za Barabarani Namanyere – Nkasi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi tayari imebainisha eneo rasmi kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa katika Mji wa Namanyere. Eneo hilo limepimwa na lina ukubwa wa takribani mita za mraba 14,678.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu na mahitaji ya wananchi wa Namanyere, Halmashauri imejenga jengo dogo la kupumzikia abiria katika eneo hilo, sambamba na kuingia mikataba na wafanyabiashara waliowekeza kwa kujenga vibanda vya biashara vinavyozunguka eneo la stendi. Hadi sasa, vibanda 88 vimejengwa na vinatoa huduma kwa wananchi, wakati jitihada za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa zikiendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa halmashauri inaendelea na ukamilishaji wa andiko la mradi ambalo litatumika kuwasilisha maombi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi hiyo ya kisasa.

Mheshimiwa Spika, suala la taa za barabarani katika Mji wa Namanyere, TARURA Wilaya ya Nkasi imewasilisha tathmini ya shilingi milioni 630, kwa ajili ya uwekaji wa taa za barabarani 196 kwenye barabara zote za lami mjini Namanyere.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa stendi pamoja na kufunga taa kwenye maeneo yaliyokidhi vigezo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini, ikiwemo barabara za Mji wa Namanyere.