Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza: - Je, mafunzo gani yanatolewa na Serikali kwa Wanawake kuhusu usimamizi wa biashara za uchukuzi na mbinu bora za usafirishaji?
Supplementary Question 1
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali madogo wawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza. Je, kuna ufuatiliaji au tathmini ya mafanikio haya yanayotolewa na Wizara kwa wanawake hawa wajasiliamali? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kufuatia ufinyu na idadi ndogo ya wanawake wajasiriamali katika fursa zinazotokana na uchukuzi, je, Wizara inachukua hatua gani kukabiliana na changamoto hii hasa katika upatikanaji wa taarifa na mitandao ya biashara? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi kwa kutambua umuhimu mkubwa wa nafasi ya mwanamke katika jamii, imeendelea kufuatilia na kuratibu kuhakikisha kwamba mwanamke kama kiongozi, kama mwanamama anakuwa sehemu muhimu ya kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za usafirishaji katika nchi yetu. Hivi ninavyozungumza tayari kozi mbalimbali kama nilivyozungumza zinaendelea kutolewa na tathmini imefanyika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya ajira milioni 16.3, wanawake ni takribani 3,200,000. Ninawahakikishia Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea kuhamasisha na kuhakikisha kwamba wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika shughuli mbalimbali za usafirishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, Mheshimiwa Mbunge ameuliza swali la pili kuhusiana na jinsi Wizara ilivyojipanga. Kwanza, tumejipanga kuhakikisha kwamba Ilani ya CCM, Toleo la 2025 ambayo imeelezea vilivyo katika Ibara ya 231, Kifungu cha (g) na (h), nafasi ya mwanamke na kuimarisha vituo vya mafunzo. Tutaendelea kukisimamia kifungu hicho kuhakikisha kwamba wanawake wanapata fursa hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, kwenye upande wa Kanuni za Manunuzi ya Umma, imeeleza vizuri sana kwenye Kanuni Namba 35, jinsi mwanamke anavyopaswa kupewa fursa, ambapo imeelezwa kwamba takribani 30% ya kazi au bidhaa au shughuli zitolewe kwa wanawake.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba mwanamke anashiriki ipasavyo katika kujenga uchumi wa Taifa lake kupitia sekta yetu ya usafirishaji. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved