Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Kilumbe Shabani Ng'enda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Mjini
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG'ENDA K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wananchi hususan Wafugaji wanaolisha mifugo maeneo ya hifadhi ya reli? (Makofi)
Supplementary Question 1
MHE. KILUMBE S. NG'ENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ambayo nayapongeza, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja, Serikali imefanya kazi nzuri sana ya usafiri kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma wa SGR na wananchi wote Tanzania sasa wanatamani hatua hiyo wafikie. Nini hatua ya Serikali katika kutekeleza mradi wa SGR kwenye maeneo yote nchini ikiwemo kufika Kigoma? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ni kwamba, reli ya kati kipande cha kutoka Kigoma kwenda Tabora kina changamoto kubwa na kimeanza ukarabati. Nataka kujua ni lini ukarabati huo utakamilika na kuwawezesha wananchi kuendelea kutumia reli hiyo?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru Mheshimiwa Kilumbe Ng’enda kwa maelezo yake ya awali ya kuipongeza Serikali yetu pendwa kwa kazi kubwa ambayo imefanywa katika miaka hii minne kwenye sekta ya reli.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumwarifu Mheshimiwa Kilumbe pamoja na Waheshimiwa Wabunge juu ya hatua mbalimbali ambazo Serikali imefanya katika kipindi kifupi cha miaka hii minne. Tukianza na kutoka Dar es Salaam - Morogoro mpaka Dodoma, hili halihitaji hata kulifafanua kwa sababu kila mtu anaona; tunapanda reli, tunafurahia usafiri salama na ulio mzuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumshukuru Mheshimiwa Rais wetu mpendwa ambaye ndiye anasimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo iliahidi kuhakikisha kwamba itaboresha usafirishaji katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi ninavyozungumza, naomba kumwarifu Mheshimiwa Mbunge, kutoka Makutupora – Tabora, Kilometa 368 mkandarasi yuko site tayari, na tuko asilimia 14.5, kutoka Tabora mpaka Isaka, Dkt. Samia Suluhu Hassan pia aliidhinisha na tulishasaini mkataba na mkandarasi ameshaanza kazi kilometa 165, tuko asilimia sita. Aidha, kutoka Mwanza mpaka Isaka kilometa 341, tuko 60%. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama haitoshi, hivi karibuni mwaka jana pia Mheshimiwa Rais alikubali, tumeanza ujenzi wa reli ya kisasa, kilometa 506 na tuko asilimia sita. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka huu mwezi wa Tatu, tumesaini mkataba unaounganisha nchi yetu kutoka Uvinza kwenda Msongati kwenye madini ya Nickel ambapo ni kilometa 240. Hii ni hatua kubwa ambayo tumeshaifanya kama Serikali kwa upande wa SGR. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hilo, tupo kwenye maandalizi kwa sababu tunao mpango kama Serikali kuhakikisha tunajenga SGR (reli ya kisasa) kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay inayounganisha pamoja na matawi la Liganga na Mchuchuma.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, tunao mpango wa kujenga reli tena kutoka Tanga mpaka Musoma ili kuunganisha na maeneo yenye machimbo au madini ikiwemo na Engaruka ambako tuna Magadi Soda, pale Minjingu tuna Phosphates na kule Dutwa tuna Nickel. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili anataka kufahamu hatua ambayo Serikali imefanya katika ujenzi wa Meter gauge kutoka Tabora kwenda mpaka Kigoma. Kwanza, nimwambie Mheshimiwa Mbunge, Serikali tayari imeshasaini mkataba na mjenzi ameanza kazi kutoka Kaliua mpaka Mpanda kilometa 210, ambapo zaidi ya bilioni 379 zimeidhinishwa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa ili kuhakikisha kwamba ukanda huo unakwenda kuboreshwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, ninavyozungumza hapa, tumeshasaini mkataba wa reli kutoka Tabora mpaka Kigoma na tunasubiri mkandarasi aweze kuanza kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamwomba Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine wa Kigoma wawe na subira, siyo muda mrefu neema inaendelea kuja kwao. (Makofi)
Name
Venant Daud Protas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igalula
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG'ENDA K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wananchi hususan Wafugaji wanaolisha mifugo maeneo ya hifadhi ya reli? (Makofi)
Supplementary Question 2
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Katika Reli ya MGR, Station ya Goweko ilikuwa ina njia tatu, lakini mlitoa njia ya pili na ya tatu mkaacha njia moja, na pale tuna mizigo mingi. Ni lini mtarudisha reli ile ili wananchi wa Goweko wapate fursa ya kupakia mizigo yao? (Makofi)
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nikae na Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kufuatilia jambo analolizungumza niweze kulifanyia kazi kwa ufasaha zaidi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved