Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza: - Je, Serikali imefikia wapi katika utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Manispaa – Moshi Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu hayo mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza. Kwa kuwa kuna Halmashauri kama Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ambayo imepata magari kutoka miji dada ambayo ni marafiki kutoka Ujerumani na kuna Halmashauri ambazo zimenunua magari haya, je, Serikali inaweza ikatoa kauli sasa kwamba umiliki wa magari haya uwe kwenye jina la Halmashauri husika?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa Azimio lilipita mwezi wa Sita mwaka 2024 na bado kama siku kumi hivi tufikishe mwaka, Mheshimiwa Waziri anaweza kututhibitishia kwamba sasa wataharakisha kukutana na Wizara zile nyingine zote ili Azimio hili liweze kusonga mbele? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, pale ambapo Manispaa husika ama halmashauri imenunua gari la zimamoto na uokoaji, umiliki utabaki kwake kwenye Halmashauri husika au Manispaa husika, lakini matengenezo na uendeshaji utasimamiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa sababu ndiyo wenye wataalam.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusu Azimio, Serikali imekuwa ikiheshimu sana Maazimio ya Bunge na imekuwa ikiyatekeleza. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, hata Azimio hili pia Serikali itajipanga, itakaa kuhakikisha kwamba Azimio hili linatekelezwa kwa ajili ya Manispaa ya Moshi na maeneo mengine hapa nchini. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza: - Je, Serikali imefikia wapi katika utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Manispaa – Moshi Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Katika Mkoa wa Manyara ambako Mheshimiwa Naibu Waziri anatoka kuna magari machache sana ya Zimamoto hasa maeneo ya Mbulu Vijijini, Mjini na hata Hanang, kuna tatizo, kukitokea kitu kinachoitwa ajali ya moto tunashindwa kupata hayo magari. Je, ni nini mpango wa Serikali katika kuyaokoa maeneo haya kwa kuletewa magari ya zimamoto?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tayari imeshanunua magari ya Zimamoto na Uokoaji kama tulivyoeleza mara nyingi hata kwenye hotuba yetu jana kwamba, magari 150 yameshanunuliwa na yatawasili nchini kwa awamu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tayari awamu ya kwanza imeshaingia mwezi huu wa Tano; na yatakapoingia, kila Wilaya hapa nchini ikiwemo Wilaya ya Mbulu na Wilaya ya Hanang’ kama alivyotaja Mheshimiwa Mbunge pia zitapata magari ya Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya shughuli za uokoaji. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved