Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 33 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 429 | 2025-05-27 |
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza: -
Je, Serikali imefikia wapi katika utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Manispaa – Moshi Mjini?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji imepanga kukutana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Wizara ya Maji na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya masuala ambayo yatawezesha utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu ushirikiano baina ya Manispaa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika shughuli za uokoaji nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea na ushirikiano baina yake na Manispaa katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa magari ya zimamoto na uokoaji, kupanga miji, upitishaji wa michoro ya ujenzi, usimikaji wa fire hydrants na upatikanaji wa viwanja vya ujenzi wa vituo vya zimamoto na uokoaji nchini ikiwemo Manispaa ya Moshi Mjini, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved